-
Dozi zaidi ya milioni 16 za chanjo ya corona kuingizwa nchini Iran hivi karibuni
Jan 25, 2021 09:16Mkuu wa kamati ya afya na tiba ya Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran amesema, taratibu zinakamilishwa kwa ajili ya kuingiza nchini dozi 16,800,000 za chanjo ya corona kutoka nchi zenye kuaminika na zilizokubalika.
-
Polisi Sudan wakabiliana na waandamanaji wanaolalamikia ughali wa maisha
Jan 25, 2021 04:09Polisi nchini Sudan wamelazimika kutumia gesi ya kutoa machozi kuwatawanya waandamanaji waliokuwa na hasira katika mji mkuu Khartoum ambao walikuwa wanalalamikia ugali wa maisha.
-
Wapalestina: Iran ndiye muungaji mkono mkuu wa ukombozi wa Palestina
Jan 24, 2021 23:01Harakati ya Jihadul Islami ya Palestina imesema kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ndiye muungaji mkono mkuu wa ukombozi wa Palestina na muqawama wa taifa hilo mbele ya jinai za utawala wa Kizayuni.
-
Waziri wa Afya wa Iran: Utoaji chanjo ya corona nchini utaanza hivi karibuni
Jan 24, 2021 10:31Waziri wa Afya, Tiba na Mafunzo ya Utabibu ya Iran amesema, utoaji chanjo ya corona hapa nchini utaanza hivi karibuni.
-
Rouhani: Iran kuanza kutoa chanjo ya Covid-19 ndani ya siku chache zijazo
Jan 23, 2021 08:42Rais Hassan Rouhani wa Iran amesema Jamhuri ya Kiislamu itaanza kutoa chanjo ya kukabiliana na ugonjwa wa Covid-19 hapa nchini katika kipindi cha siku chache zijazo.
-
Zarif: Mlango wa fursa kwa utawala mpya wa Marekani hautabaki wazi milele
Jan 23, 2021 08:19Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amemuasa Rais mpya wa Marekani Joe Biden, ahitimishe sera za mashinikizo zilizogonga mwamba za mtangulizi wake Donald Trump na kusisitiza kuwa, "dirisha la fursa kwa timu mpya ya Ikulu ya White House halitabakia wazi milele."
-
Iran kuanzisha kituo kikubwa zaidi cha Teknolojia nchini Kenya
Jan 23, 2021 01:36Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetangaza kuanzisha kituo kikubwa cha ubunifu na teknolojia katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi ikiwa ni katika mkakati wa kuimarisha uhusiano wa nchi hizi mbili rafiki.
-
Zaidi ya wagonjwa milioni 1 na laki 1 na 51,000 wapata afueni ya COVID-19 nchini Iran
Jan 22, 2021 08:22Msemaji wa Wizara ya Afya, Tiba na Mafunzo ya Utabibu ya Iran amesema kuwa, zaidi ya wagonjwa milioni 1 na laki 1 na 51 elfu wa COVID-19 wamepata afueni nchini Iran.
-
Zarif: Trump ametupwa katika jaa la taka za historia, jina la Soleimani litang’ara
Jan 21, 2021 01:14Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Mohammad Javad Zarif amesema rais aliyeondoka Marekani wa Marekani ametupwa katika jaa la taka za historia.
-
Zarif: Mjumbe wa Iran UN hajazungumza na Marekani
Jan 21, 2021 00:54Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Mataifa hajafanya mazungumzo yoyote na Marekani kama lilivyodai gazeti moja la Ufaransa.