-
Agizo jipya la Trump dhidi ya maafisa wa Iran na tapatapa za mfamaji
Sep 27, 2019 03:39Rais Donald Trump wa Marekani jana Alkhamisi aliendeleza sera zake za kuiweka mashinikizo ya juu zaidi kwa shabaha ya kuilazimisha Jamhuri ya Kiislamu isalimu amri mbele ya matakwa ya serikali ya Washington.
-
Iran yaitaka Uingereza iache ukhabithi na ushetani wake wa kuingilia mambo ya wengine
Sep 26, 2019 23:27Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, Uingereza inapaswa kuacha ukhabidhi na ushetani wake wa kuingilia masuala ya eneo la Mashariki ya Kati na kuwauzia silaha wavamizi wa Yemen pamoja na kushiriki katika jinai dhidi ya binadamu ambazo zimethibitishwa pia na Umoja Mataifa.
-
Rouhani: Vikwazo vya kikatili vya Marekani vimeongeza mshikamano nchini Iran
Sep 26, 2019 09:02Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema vikwazo vya kikatili vya Marekani dhidi ya Tehran vimeshindwa kufikia malengo yake, na badala yake vimeongeza mshikamano miongoni mwa wananchi wa Iran.
-
China yalaani vikwazo vya Marekani dhidi yake kwa kununua mafuta ya Iran
Sep 26, 2019 08:51Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje wa China amekosoa vikali hatua ya Marekani ya kuiwekea vikwazo vipya nchi hiyo ya Asia kwa kuendelea kununua mafuta ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
-
Muungano wa Matumaini, lugha ya amani katika kilele cha nguvu na uwezo
Sep 26, 2019 04:13Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, akiwa anawakilisha Wairani wote katika mkutano wa kila mwaka wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, amezungumza kuhusu amani na 'Muungano wa Matumaini' na wakati huo huo akatoa kauli yenye nguvu na kutahadharisha kuhusu chokochoko zozote dhidi ya Iran.
-
Rais Rouhani: Katu hatutofanya mazungumzo na adui chini ya vikwazo
Sep 25, 2019 12:52Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema ni jambo lisiloyumkinika kwa taifa hili kufanya mazungumzo na adui likiwa chini ya mashinikizo na vikwazo vya kidhalimu na vilivyo kinyume cha sheria.
-
Trump akariri tena tuhuma zake dhidi ya Iran katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa
Sep 25, 2019 01:13Rais Donald Trump wa Marekani amelitumia jukwaa la mkutano wa 74 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kukariri kwa mara nyingine tena porojo na tuhuma zake za kila siku dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
-
Zarif na Mogherini wajadili njia za kuinusuru JCPOA
Sep 24, 2019 04:29Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Mohammad Javaad Zarif amekutana na kufanya mazungumzo na Mkuu wa Sera za Kigeni wa Umoja wa Ulaya, Federica Mogherini na wawili hao wamejadili njia za kulinda na kudumisha makubaliano ya JCPOA.
-
Rouhani: Madai ya Ujerumani, Uingereza na Ufaransa dhidi Iran hayana msingi wowote
Sep 24, 2019 00:19Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amekosoa vikali tuhuma zilizotolewa na Ujerumani, Uingereza na Ufaransa kuwa eti Iran ilihusika katika mashambulizi yaliyolenga kituo kikubwa cha kusafisha mafuta cha Aramco nchini Saudi Arabia na kusisitiza kuwa, madai hayo haya msingi wowote.
-
Kukiri Marekani kwamba vikwazo vyake dhidi ya Iran vimefika kileleni na vimefeli
Sep 23, 2019 23:18Baada ya kujitoa bila sababu katika mapatano ya kimataifa ya nyuklia maarufu kwa jina la JCPOA na kuirejeshea Iran vikwazo vyote vilivyokuwa vimeondolewa baada ya mapatano hayo, bali kuongeza vikwazo vikubwa zaidi ambavyo havijawahi kutokea mfano wake, leo hii serikali ya Donald Trump ya Marekani imelazimika kukiri kuwa vikwazo vyake hivyo vimeshindwa kuzaa matunda yaliyotarajiwa.