-
Rouhani: Iran iko tayari kunyoosha mkono wa urafiki kwa jirani zake
Sep 22, 2019 04:46Rais Hassan Rouhani amesema Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ipo tayari kunyoosha mkono wa urafiki kwa jirani zake, sambamba na kusamehe makosa yaliyofanywa na baadhi ya nchi hizo.
-
Mateka Muirani aachiwa huru na maharamia wa Somalia
Sep 22, 2019 04:11Raia wa Iran ambaye amekuwa akishikiliwa mateka na maharamia wa Somalia kwa miaka kadhaa sasa hatimaye ameachiwa huru.
-
Iran kuendelea kuimarisha makombora yake ya balistiki licha ya kelele za Marekani
Sep 21, 2019 03:12Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa amesema Jamhuri ya Kiislamu ya Iran itaendelea kuimarisha mfumo wake wa makombora ya balistiki licha ya kelele za Marekani.
-
Mchezo wa Aramco; makelele ya timu ya Trump na jibu la Zarif
Sep 20, 2019 04:35Licha ya kuwa sababu ya kushambuliwa kiwanda cha kusafisha mafuta cha Aramco nchini Saudi Arabia inapasa kutafutwa katika vita vya Yemen lakini watawala wa Saudia na Marekani wanaelekeza sababu hiyo kwingine kwa kuituhumu Iran kuwa imehusika katika shambulio hilo.
-
Vikwazo dhidi ya Iran; radiamali ya Marekani juu ya kudhalilishwa Saudia katika shambulio la Aramco
Sep 20, 2019 03:34Baada ya kiwanda cha kusafisha mafuta cha Saudi Arabia Aramco, kushambuliwa kwa ndege zisizokuwa na rubani na jeshi la Yemen, kwa mara nyingine tuhuma za Marekani zimekuwa zikielekezwa kwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
-
Zarif: Vikwazo vya Marekani vinawalenga wananchi wa kawaida wa Iran
Sep 19, 2019 09:17Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amekosoa vikali hatua ya utawala wa Rais Donald Trump wa Marekani ya kutangaza vikwazo vipya dhidi ya taifa hili na kusisitiza kuwa, kushadidishwa ugaidi huo wa kiuchumi kwa mara nyingine kumeonesha namna Washington inavyowalenga Wairani wa kawaida.
-
Marekani na utumiaji wa viza kama wenzo wa mashinikizo dhidi ya washiriki katika vikao vya UN
Sep 19, 2019 06:57Marekani ambayo ni mwenyeji wa makao makuu ya Umoja wa Mataifa huko New York daima imekuwa ikitumia suala la kutoa viza kwa jumbe na maafisa wa nchi mbalimbali wanaotaka kushiriki vikao vya Umoja wa Mataifa kama wenzo wa kutoa mashinikizo dhidi ya nchi zinazopinga sera za kibeberu za nchi hiyo.
-
Safari ya Pompeo nchini Saudia na Imarati; njama za Marekani za kuzusha mizozo Mashariki ya Kati
Sep 19, 2019 02:46Mashambulio ya ndege zisizo na rubani dhidi ya taasisi za mafuta za Saudi Arabia ambayo yamepelekea kupungua kwa asilimia 50 uzalishaji mafuta wa nchi hiyo ya Kiarabu, yameiibua Marekani na kuifanya itoe radiamali kuhusiana na jambo hilo.
-
Katika mtazamo wa Kansela wa Ujerumani; Mwarubaini wa kupunguza mivutano Magharibi ya Asia ni kurejea kwenye JCPOA
Sep 18, 2019 07:25Kwa mtazamo wa Umoja wa Ulaya na Troika ya umoja huo inayoundwa na Ujerumani, Ufaransa na Uingereza, makubaliano ya nyuklia ya JCPOA yana mchango muhimu sana katika kulinda amani na usalama katika eneo la Magharibi ya Asia na katika uga wa kimataifa. Kwa mtazamo wa nchi za Ulaya, kujitoa Marekani katika JCPOA kumekuwa chanzo cha kujitokeza mivutano na hali ya wasiwasi katika Ghuba ya Uajemi na Magharibi ya Asia.
-
'Kushambuliwa vituo vya mafuta vya Saudia, kunabainisha udhaifu na kushindwa kwa Riyadh'
Sep 17, 2019 07:55Mtaalamu na mchambuzi wa masuala ya Magharibi mwa Asia amekadhibisha madai yaliyotolewa kwamba Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imehusika katika shambulizi dhidi ya taasisi za mafuta za Saudi Arabia na kusema kuwa, shambulizi hilo kwenye taasisi hizo limeonyesha udhaifu na kushindwa kwa Wasaudi.