Sep 19, 2019 13:47 UTC
  • Zarif: Vikwazo vya Marekani vinawalenga wananchi wa kawaida wa Iran

Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amekosoa vikali hatua ya utawala wa Rais Donald Trump wa Marekani ya kutangaza vikwazo vipya dhidi ya taifa hili na kusisitiza kuwa, kushadidishwa ugaidi huo wa kiuchumi kwa mara nyingine kumeonesha namna Washington inavyowalenga Wairani wa kawaida.

Katika ujumbe katika ukurasa wake rasmi wa mtandao wa kijamii wa Twitter, Muhammad Javad Zarif amesema, "Katika kushadidisha vita vya kiuchumi dhidi ya Wairani, Donald Trump amemuagiza Waziri wa Fedha kulibana zaidi taifa la Iran. Huko ni kukiri wazi kuwa Marekani inawalenga wananchi wa kawaida kwa makusudi katika ugaidi wake wa kiuchumi ambao ni kinyume cha sheria na kitendo kisichokuwa cha kibinadamu."

Dakta Zarif amesema hatua hiyo ya Trump inakusudia kushadidisha vita vya kiuchumi dhidi ya Tehran pasina kujali matokeo yake. 

Rais wa Marekani amemuagiza Waziri wa Fedha wa nchi hiyo, Steven Mnuchin kuiwekea Iran vikwazo vikali kufuatia kushindwa siasa za mashinikizo ya juu zaidi za Marekani dhidi ya nchi hii.

Mike Pompeo, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Marekani akiwa katika mazungumzo na Muhammad bin Salman, mrithi wa kiti cha ufalme wa Saudi Arabia

Trump ametangaza vikwazo hivyo vipya dhidi ya Iran kwa shabaha ya kuiahadaa Saudia, ambayo inajaribu kujikusanya na kuponya makovu ya kipigo kikali kutoka vikosi vya Yeme.

Jumamosi iliyopita, kikosi cha ndege zisizo na rubani cha Yemen kwa kushirikiana na kamati za wananchi, kilitumia ndege 10 zisizo na rubani (drone) zilizotengezwa na Wayemen, kushambulia vituo vya kusafisha mafuta vya Buqayq na Khurais, vinavyomilikiwa na Shirika la Kitaifa la Mafuta la Saudia ARAMCO na kusababisha hasara kubwa kwa Riyadh.

Tags