Iran yatungua droni na ndege nyuki 44 katika kipindi cha masaa 48
(last modified Sun, 15 Jun 2025 11:14:16 GMT )
Jun 15, 2025 11:14 UTC
  • Iran yatungua droni na ndege nyuki 44 katika kipindi cha masaa 48

Kamanda wa Kikosi cha Ulinzi wa Mipakani, Brigedia Jenerali Ahmad Ali Goodarzi, amesema kuwa, Iran imefanikiwa kutungua droni (ndege isiyo na rubani) na ndege nyuki 44 za adui Mzayuni kiatika kiipindi cha masaa 24 yaliyopita.

Afisa huyo wa kijeshi amesema, kutokana na umakini wa walinzi shupavu na wenye ghera wa Mipaka ya Faraja, ndege 44 zisizo na rubani na ndege ndogo nyuki za utawala wa Kizayuni zilionekana na kuharibiwa katika baadhi ya mipaka ya nchi hii.

Aidha amesema, kufuatia shambulio hilo la anga la utawala ghasibu wa Israel, katika muda wa saa 48 zilizopita, ndege 44 zisizo na rubani na ndege ndogo ndogo za utawala huo zilizojaribu kuingia katika anga ya Iran zilifuatiliwa na kuharibiwa.

Akigusia utayarifu wa 100% wa kiutendaji wa askari wa mpakani katika kudhibiti na kulinda mipaka ya Iran ya Kiislamu Brigedia Jenerali Ahmad Ali Goodarzi ameongeza kuwa: "Vikosi vya ulinzi wa mpaka na ambavyo viko tayari kufa kwa ajili ya kulinda mi9paka ya nchi huko Farajah vimeyaonya makundi yote yenye uadui, kigaidi, yenye silaha na wasafirishaji wa magendo kwamba vitajibu kwa nguvu mashambulizi yoyote katika mipaka ya taifa hili.

Kamanda wa Kikosi cha Walinzi wa Mipakani sambamba na kutangaza mshikamano kamili na vikosi vingine vya jeshi, amesisitiza kuwa, mamlaka husika ziko macho na zina udhibiti kamili wa kiinteliijensia, na kuuna azma thabiti ya walinzi wa mpakani katika kudumisha usalama wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kukabiliana na vitisho vyovyote katika ukanda wa mpaka.