Mufti wa Oman ataka Waislamu wote kuiunga mkono Iran
(last modified Sat, 14 Jun 2025 10:49:32 GMT )
Jun 14, 2025 10:49 UTC
  • Mufti wa Oman ataka Waislamu wote kuiunga mkono Iran

Sheikh Ahmed bin Hamad al-Khalili, Mufti wa Oman amesema katika ujumbe kwenye mtandao wa kijamii wa X kwamba: "Tuna imani Mwenyezi Mungu atavipa ushindi Vikosi vya Uliinzi vya Iran."

Vilevile Mufti al Khalili amesisitiza kwa kusema: "Muislamu ni ndugu wa Muislamu mwenzake, hamuui, hamsalimishi kwa adui na hamvunji moyo."

Mufti Mkuu wa Oman, Sheikh Ahmad bin Hamad al Khalili ametoa tamko hilo muhimu kufuatia mashambulizi ya kigaidi ya Israel dhidi ya taifa ndugu na rafiki la Iran.

Amesema: Tumeshtushwa na kuhuzunishwa na uadui wa utawala katili wa Kizayuni dhidi ya Iran. Lakini pamoja na hayo, tuna yakini kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu atalinusuru taifa hilo la Kiislamu (Iran). Na hakuna nusra isipokuwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu, Mwenye nguvu, Mwenye hikma.

Kabla ya hapo pia, Mufti wa Oman aliwahi kuipongeza Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa kutoa majibu makali kwa Israel wakati wa operesheni ya kulipiza kisasi iliyofanywa na Iran ya kuyapiga kwa makombora maeneo nyeti ya utawala wa Kizayuni baada ya utawala huo kuua wanadiplomasia wa Iran nchini Syria.

Katika taarifa yake hiyo aliyoituma kwenye mtandao wa kijamii wa X, Sheikh Ahmed bin Hamad Al Khalili alisema: Hiki tunachokiona kwenye vyombo vya habari kuhusu jibu la kijasiri la Iran dhidi ya utawala wa Kizayuni kinamfurahisha mtu.

"Tunashukuru kwa hatua hii ya Iran na tunasubiri kuona ni nini kitakachovunja nguvu za Wazayuni na waungaji mkono wao na kuwasaidia Waislamu," aliongeza.

Mufti Mkuu wa Oman alisema pia kwamba, hatua hiyo ya kupongezwa ya Iran ya kuushambulia moja kwa moja utawala wa Kizayuni katika operesheni ya kulipiza kisasi, itawazuia Wazayuni kukandamiza raia wa Palestina hususan wa Ukanda wa Ghaza.