-
Iran: US, Israel ziliwapa silaha, fedha wafanya ghasia nchini
Jan 16, 2026 02:54Waziri wa Ulinzi wa Iran amesema Marekani na Israel zilipanga na kufanikisha ghasia zilizoshuhudiwa hapa nchini hivi karibuni, zikielekeza silaha na pesa taslimu kuchochea vurugu na uvunjifu wa utulivu, ikiwa ni sehemu ya mpango mpana wa kuibua mgawanyiko na mifarakano katika taifa hili.
-
Iran yatangaza siku tatu za kuwaomboleza waliouawa shahidi katika jinai zilizochochewa na US na Israel
Jan 12, 2026 06:39Serikali ya Iran imetangaza siku tatu za maombolezo kwa ajili ya kuwakumbuka waathiriwa, wakiwemo askari wa vikosi vya usalama na wa jeshi la kujitolea, ambao wameuliwa shahidi na wafanyaji fujo na vurugu wanaoungwa mkono na Marekani na utawala wa kizayuni wa Israel, waliojaribu kuteka nyara maandamano ya amani ya wananchi ya kulalamikia hali ya uchumi nchini.
-
Ripoti: Israel inapanga kuanzisha mashambulizi mapya dhidi ya Ghaza ifikapo mwezi Machi
Jan 12, 2026 06:02Gazeti la Kizayuni la Times of Israel limeripoti kuwa, jeshi la utawala haramu wa Israel linapanga kuanzisha mashambulizi mapya dhidi ya Ukanda wa Ghaza ifikapo mwezi Machi ili kunyakua ardhi zaidi za eneo hilo na kuusukuma Mstari wa Njano kuelekea magharibi zaidi upande wa pwani ya eneo hilo.
-
Kiongozi wa upinzani Bahrain ahukumiwa kifungo jela, atozwa faini kwa kuikosoa Israel
Jan 12, 2026 06:02Wanaharakati nchini Bahrain wameelezea wasiwasi walionao kuhusu hatima ya kiongozi wa upinzani Ebrahim Sharif baada ya kuhukumiwa kifungo cha miezi sita jela kwa kukosoa uhusiano wa utawala wa kifalme wa nchi hiyo na utawala wa kizayuni wa Israel.
-
Somalia: Israel kuwahamishia kwa nguvu Wapalestina Somaliland ni kinyume cha sheria za kimataifa
Jan 11, 2026 06:56Waziri wa Ulinzi wa Somalia, Ahmed Moalim Fiqi, ameishutumu Israel kwa kupanga kuwahamisha kwa nguvu Wapalestina wa Ukanda wa Gaza na kuwapeleka katika eneo lililojitenga la Somaliland, akiukashifu mpango huo alioutaja kuwa ni "ukiukaji mkubwa" wa sheria za kimataifa.
-
Mashambulizi ya Wazayuni dhidi ya Msikiti wa al Aqsa yaliongezeka sana mwaka 2025
Jan 10, 2026 06:42Duru za Palestina zimeripoti kwamba mashambulizi ya walowezi wa Kizayuni dhidi ya Msikiti wa al Aqsa huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu na kuvunjia heshima eneo hilo takatifu yaliongezeka kwa kiwango kikubwa katika mwaka uliomalizika majuzi wa 2025 na kwamba mashambulizi hayo yaliandamana na ujumbe wa kisiasa na kidini.
-
"Handala" yafichua operesheni za MOSSAD ndani ya Iran
Jan 09, 2026 06:23Kundi moja la kutetea Palestina linalofahamika kwa jina la Handala limefichua utambulisho wa Mehrdad Rahimi, mtu anayeelezwa kuwa afisa wa kusimamia na kuendesha operesheni za maajenti wa shirika la kijasusi la Israel la Mossad hapa nchini Iran.
-
Wizara ya Afya ya Palestina: Waliouawa shahidi Gaza ni zaidi ya 71,300
Jan 09, 2026 06:23Wizara ya Afya ya Palestina imeeleza katika takwimu zake za hivi karibuni kwamba, Wapalestina zaidi ya 71,000 wameuawa shahidi katika vita vya mauaji ya kimbari vilivyoanzishwa na utawala wa kizayuni wa Israel dhidi ya Ukanda wa Gaza Oktoba 2023.
-
Utafiti: Takriban asilimia 90 ya watu katika nchi za Kiarabu wanapinga kuanzishwa uhusiano na Israel
Jan 09, 2026 02:22Idadi kubwa ya watu katika Ulimwengu wa Kiarabu wanapinga kuitambua Israel na kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala huo ghasibu. Hii ni kwa mujibu wa uchunguzi mpya wa maoni wa kikanda.
-
UN yaitaka Israel ikomeshe 'mfumo wa ubaguzi wa apathaidi' inaoendesha Ukingo wa Magharibi
Jan 08, 2026 03:05Umoja wa Mataifa kupitia Kamishna wake Mkuu wa Haki za Binadamu umesema, hatua za miongo kadhaa za Israel za kuwatenga na kuwabagua Wapalestina katika Ukingo wa Magharibi inaoukalia kwa mabavu zinazidi kuongezeka, na kwa sababu hiyo umetoa wito wa kuutaka utawala huo ukomeshe "mfumo wake wa ubaguzi wa rangi wa apathaidi".