Iran: US, Israel ziliwapa silaha, fedha wafanya ghasia nchini
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i135534-iran_us_israel_ziliwapa_silaha_fedha_wafanya_ghasia_nchini
Waziri wa Ulinzi wa Iran amesema Marekani na Israel zilipanga na kufanikisha ghasia zilizoshuhudiwa hapa nchini hivi karibuni, zikielekeza silaha na pesa taslimu kuchochea vurugu na uvunjifu wa utulivu, ikiwa ni sehemu ya mpango mpana wa kuibua mgawanyiko na mifarakano katika taifa hili.
(last modified 2026-01-15T23:24:29+00:00 )
Jan 15, 2026 23:24 UTC
  • Rais Donald Trump
    Rais Donald Trump

Waziri wa Ulinzi wa Iran amesema Marekani na Israel zilipanga na kufanikisha ghasia zilizoshuhudiwa hapa nchini hivi karibuni, zikielekeza silaha na pesa taslimu kuchochea vurugu na uvunjifu wa utulivu, ikiwa ni sehemu ya mpango mpana wa kuibua mgawanyiko na mifarakano katika taifa hili.

Brigedia Jenerali Aziz Nasirzadeh alisema hayo jana Alkhamisi na kuongeza kwamba, Iran ina "taarifa sahihi za kiintelijensia" zinayoonyesha Marekani, utawala wa Israel, na baadhi ya nchi waitifaki wao waliunda vituo vya pamoja vya uratibu ili kuunda mustakabali wa "wanaotaka kujitenga" na magaidi.

Amesema mikutano kadhaa ya maafisa wa Marekani, Israel na waitifaki wao ilifikia hatua ya kupanga kila "eneo litakalojitenga" kuunda katiba yake, huku wafadhili wa kigeni wakipewa jukumu la kufanya magendo ya silaha na kutoa usaidizi wa kifedha na vifaa.

Brigedia Jenerali Nasirzadeh amesema idara za kiintelijensia za Iran zina habari kamili juu ya mipango hii, ikiwa ni pamoja na vikao vya pamoja vilivyofanyika katika moja ya nchi katika eneo hili kwa lengo la kuwasha na kuchochea moto wa "machafuko" ndani ya Iran.

Kwa mujibu wa kamanda huyo, idara za kijasusi za Marekani na nchi kadhaa za Magharibi ziliwasilisha "programu zao maalum za kuongeza bajeti" kwa ajili ya kuyumbisha utulivu wakati wa mikutano hiyo.

Amefichua kuwa, mikutano hiyo ilipasisha hata "malipo" vya uharibifu na mauaji ndani ya Iran. Amesema, "Kwa kuua mtu mmoja, (malipo yake ni) toman milioni 500 (takriban dola 3,300 za Marekani). Kwa kuchoma kila gari, toman milioni 200 (takriban dola 1,300 za Marekani). Kwa kuchoma vituo vya polisi, toman milioni 80 (takriban dola 530 za Marekani). Na kwa hatua yoyote ya uharibifu na vurumai, toman milioni 15 (takriban dola 100 za Marekani)."