"Handala" yafichua operesheni za MOSSAD ndani ya Iran
Kundi moja la kutetea Palestina linalofahamika kwa jina la Handala limefichua utambulisho wa Mehrdad Rahimi, mtu anayeelezwa kuwa afisa wa kusimamia na kuendesha operesheni za maajenti wa shirika la kijasusi la Israel la Mossad hapa nchini Iran.
Shirika la habari la Iran Press limeripoti habari hiyo na kueleza kuwa, kundi hilo la udukuzi la Handala limeanika shughuli za maajenti wa Mossad hapa nchini Iran, ikiwemo kuwasha na kuchochea moto wa ghasia wakati wa maandamano ya wafanyabiashara hapa nchini.
Kadhalika Handala imefichua ushirikiano wa karibu uliopo baina Rahimi, raia anayejiita mwanastratejia wa operesheni za maajenti wa Mossad hapa nchini na mashirika ya kiusalama ya utawala wa Kizayuni.
Idadi ya majasusi walionyongwa kwa kupatikana na hatia ya kufanya ujasusi kwa maslahi ya Israel iliongezeka mwaka uliopita nchini Iran, hasa kabla na baada ya vita vya siku 12 vya mwezi Juni.
Ripoti zinaonyesha kwamba, zaidi ya majasusi 700 waliokuwa wakishirikiana na Mossad wamekamatwa kote nchini Iran baada ya uvamizi wa Israel dhidi ya nchi hii mwezi Juni.
Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mpaka sasa imeshatekeleza hukumu ya kifo dhidi ya maajenti kadhaa waliopatikana na hatia ya kushirikiana na shirika la kijasusi la utawala wa Israel Mossad, kwa kutoa taarifa nyeti kuhusu maeneo ya kiusalama ya Iran.
Itakumbuwa kuwa, Aprili mwaka jana 2025, kundi la kuwatetea wananchi madhulumu wa Palestina la Handala lilifanikiwa kujipenyeza na kudukua mifumo ya rada ya jeshi la Israel, na kuulemeza mfumo unaopigiwa debe wa ulinzi wa anga wa Israel wa Kuba la Chuma 'Iron Dome'.