-
Kamanda Hajizadeh: Operesheni ya SEPAH ni mwanzo wa mchakato wa kutoka wanajeshi wa Marekani Asia Magharibi
Jan 10, 2020 00:36Kamanda wa Kikosi cha Anga za Mbali cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH amezungumzia mashambulizi ya makombora yaliyofanywa na jeshi hilo kwenye kambi za wanajeshi magaidi wa Marekani nchini Iraq na kuongeza kuwa, thamani ya damu ya shahid Luteni Jenerali Qassem Soleimani ni kufukuzwa kikamilifu wanajeshi wa Marekani katika eneo hili, na shambulio hilo la SEPAH ndio mwanzo wa mchakato huo.
-
Rais Rouhani: Umoja wa Ulaya unapaswa kuwa na misimamo huru, usiburuzwe na Marekani
Jan 10, 2020 00:36Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, mahesabu ghalati na yenye madhara makubwa ya Marekani yanatokana na kushindwa nchi hiyo kuielewa vizuri Iran na eneo la Asia Magharibi. Amesisitiza kuwa, Umoja wa Ulaya unapaswa kuwa huru na usikubali kuburuzwa na Marekani na kuifanya Iran ikate tamaa kikamilifu na umoja huo.
-
Newsweek: Wanajeshi 270 wa Marekani wameuawa katika mashambulio ya SEPAH
Jan 10, 2020 00:34Kwa mara ya kwanza toleo la mtandao la gazeti la kila wiki la Newsweek la Marekani limefichua kwamba, kwa uchache wanajeshi 270 wa nchi hiyo wameangamizwa katika shambulio la usiku wa kuamkia Jumatano lililofanywa na Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH katika kambi mbili za Marekani za Ain al Asad na Erbil nchini Iraq.
-
Majibu ya kutapatapa ya Trump baada ya Iran kupiga kwa makombora kambi za Marekani + Video
Jan 09, 2020 10:50Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetekeleza kivitendo ahadi yake ya kutoa jibu kali kwa jinai ya Marekani ya kumuua kigaidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda Mkuu wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH.
-
Onyo kali la Muqtada al-Sadr na kuwa pamoja makundi yote ya muqawama nchini Iraq dhidi ya Marekani
Jan 09, 2020 01:15Moja ya matokeo muhimu ya jinai ya serikali ya kigaidi ya Marekani ya kumuua shahidi Luteni Jenerali Qassim Soleimani na Abu Mahdi al-Mohandes na watu wanane waliokuwa wamefuatana nao ni kujitokeza hali ya umoja baina ya makundi ya muqawama nchini Iraq dhidi ya Marekani.
-
Kiongozi Muadhamu: Tumempiga kibao tu adui, anachopaswa kufanya Marekani ni kuondoka eneo hili
Jan 08, 2020 13:09Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa, mashambulio ya makombora yaliyofanywa na Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH katika kambi mbili za Marekani nchini Iraq ni kibao cha uso tu alichopigwa adui huyo.
-
Rouhani: Majibu kamili ya Iran ni kukatwa miguu ya Wamarekani Asia Magharibi
Jan 08, 2020 11:33Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amegusia majibu makali yaliyotolewa usiku wa kuamkia leo na Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH ya kuwashambulia magaidi wa Kimarekani katika kambi zao mbili za kijeshi nchini Iraq na kusema kuwa, majibu kamili ya Iran kwa jinai za Wamarekani ni kukatwa miguu yao kwenye eneo hili.
-
Meja Jenerali Baqeri: Tutatoa jibu kali zaidi kwa hatua yoyote ovu ya US
Jan 08, 2020 08:04Mkuu wa Vikosi vya Ulinzi vya Iran amesema kuwa, majeshi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran yatatoa jibu kali zaidi na kwa nguvu zote dhidi ya hatua yoyote ghalati na ovu ya Marekani.
-
Iran yavurumisha makombora ya balestiki na kupiga kambi za jeshi za Marekani
Jan 08, 2020 03:48Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) limevurumisha makombora ya balestiki na kupiga kambi za kijeshi za Marekani nchini Iraq, kama jibu la kuuawa shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, aliyekuwa Kamanda wa Kikosi cha Quds cha SEPAH.
-
Kamanda wa IRGC: Tutalipiza kisasi cha kuuawa shahidi Jenerali Soleimani
Jan 07, 2020 08:16Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kisasi cha taifa la Iran kwa damu ya kuuawa shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda Mkuu wa Kikosi cha Quds cha SEPAH kitakuwa kikali, madhubuti, cha kutisha na kamilifu.