Idara ya Ujasusi wa Nje ya Russia (SVR) imesema katika taarifa yake ya siku ya Ijumaa kwamba Marekani inawapa mafunzo magaidi wa Daesh (ISIS) katika kituo cha Al-Tanf nchini Syria ili wapelekwe Ukraine.
Ayatullah Naser Makarem Shirazi, mmoja wa wanazuoni wakubwa wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, amesema kuwa, hii leo ulimwengu wa Kiislamu unakabiliwa na hatari ya fikra za ukufurishaji.
Mkuu wa Baraza la Utendaji la Harakati ya Kiislamu ya Hizbullah nchini Lebanon, amesema kuwa kushindwa mradi kabambe wa makundi ya ukufurishaji na Kiwahabi katika eneo la Mashariki ya Kati, kumetokana na mafundisho bora ya Imamu Ruhullah Komein (MA) Mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na pia miongozo ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei.
Rais Hassan Rouhani amesema uenezaji hofu na chuki dhidi ya Uislamu (Islamophobia), ubaguzi wa rangi na fikra za ukufurishaji chimbuko lao ni moja.
Duru za Yemen zimeripoti kuwa, ndege moja ya Uturuki imewahamishia nchini humo makumi ya magaidi wa Daesh (ISIS) kwa kutumia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Aden, kusini mwa Yemen, baada ya magaidi hao kufurushwa nchini Syria.
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kukurubisha Pamoja Madhehebu za Kiislamu amesema kuwa, harakati ya utakfiri katika njama zake imeulenga utambulisho mmoja wa jamii ya Kiislamu.
Rais Vladimir Putin wa Russia amekosoa sera za nchi za Magharibi za kuyatumia makundi ya kigaidi kama wenzo wa kufikia malengo yao na kusisitiza kuwa mchezo huo mchafu umesababisha matatizo mengi.
Kiongozi wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Lebanon, Hizbullah, amesema anaitazama itikadi ya misimamo mikali ya Uwahhabi kuwa hatari zaidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel.
Rais Hassan Rouhani wa Iran ametoa wito kwa nchi za Waislamu dunaini kuungana na kuuwajibisha utawala wa Saudia kutokana na jinai zake katika nchi za Waislamu eneo la Mashariki ya Kati.