Mji wa Jiaxing ulioko mashariki mwa China jana uliidhinisha matumizi ya chanjo ya virusi vya corona ya CoronaVac ambayo imeingizwa sokoni na kuanza kuuzwa kwa gharama ya dola 60 za kimarekani.
Russia imetangaza leo Jumamosi kwamba imeanza kuzalisha chanjo ya virusi vya corona (COVID-19) kwa ajili ya matumizi ya umma huku nchi mbalimbali duniani zikizidisha juhudi za kudhibiti maambukizi ya virusi hivyo.