-
Iran: Tutatoa jibu madhubuti kwa azimio la US, EU lililopasishwa na IAEA dhidi yetu
Jun 09, 2022 18:52Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amelaani kitendo cha Bodi ya Magavana ya Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki IAEA cha kupasisha azimio dhidi ya Tehran na kusisitiza kuwa, taifa hili litatoa jibu mwafaka na madhubuti kwa hatua hiyo.
-
Mama ashtakiwa Marekani baada ya mtoto wa miaka 2 kumuua baba kwa kumpiga risasi
Jun 07, 2022 23:08Mwanamke mmoja katika mji wa Orlando jimboni Florida nchini Marekani ameshtakiwa kwa kosa la kumuua mumewe bila kukusudia baada ya mtoto wao wa miaka miwili kufyatua risasi kwa bahati mbaya ndani ya nyumba yao iliyompata mgongoni baba mtu na kumuua.
-
New York Post: Los Angeles ni kitovu cha wizi wa kutumia silaha Marekani
Jun 05, 2022 03:32Gazeti la New York Post limeripoti kuwa mji wa Los Angeles umegeuka kuwa moja ya vitovu vya wizi wa kutumia silaha nchini Marekani na kwamba magenge wa wezi wanaotumia nguvu yamekuwa tishio kubwa kwa raia na nyumba zao.
-
Sisitizo la Katibu Mkuu wa NATO kuhusu kujiandaa Magharibi kwa vita vya muda mrefu Ukraine
Jun 04, 2022 22:08Katibu Mkuu wa Jeshi la Nchi za Magharibi NATO, Jens Stoltenberg, baada ya kuonana na rais wa Marekani, Joe Biden ili kujua msimamo wa Washington kuhusu vita vya Ukraine amedai kwamba nchi za Magharibi zinapaswa kujiandaa kwa vita vya muda mrefu huko Ukraine.
-
Kuwait yachukizwa na hatua ya balozi wa Marekani kutetea maingiliano ya kimwili ya watu wa jinsia moja
Jun 03, 2022 23:43Wizara ya Mambo ya Nje ya Kuwait imemwita balozi mdogo wa Marekani nchini humo kufuatia hatua ya ubalozi wao kutoa matamshi ya kutetea na kuunga mkono maingiliano ya kimwili ya watu wa jinsia moja.
-
Medvedev: Russia iko kwenye vita vinavyopiganwa kwa niaba ya Marekani na Ulaya
Jun 03, 2022 23:37Mkuu wa Baraza la Usalama wa Taifa la Russia amesema, nchi yake iko kwenye vita vinavyopiganwa kwa niaba ya Marekani na Ulaya na akasisitiza kuwa kuna ulazima wa kuzuia kutokea vita vya atomiki.
-
Iran yazionya Marekani na nchi tatu za Ulaya
Jun 01, 2022 22:53Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ya Iran amezihutubu nchi tatu za Ulaya, yaani Ujerumani, Uingereza na Ufaransa pamoja na Marekani na kusema: "Mnaweza kufuata mkondo wa udiplomasia au muende kinyume chake. Sisi tuko tayari kwa machaguo hayo mawili."
-
IRGC: Meli mbili za mafuta za Ugiriki zimekamatwa katika maji ya Ghuba ya Uajemi kwa kukiuka taratibu
May 27, 2022 22:45Idara Kuu ya Mahusiano ya Umma ya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) imetangaza kuwa meli mbili za mafuta za Ugiriki zimekamatwa katika maji ya Ghuba ya Uajemi kwa sababu ya kukiuka taratibu.
-
Iran yakosoa mitazamo ya upande mmoja na taathira zake hasi kwa utulivu wa eneo na usalama wa kimataifa
May 26, 2022 21:53Awamu ya tatu ya mazungumzo ya kisiasa kati ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Italia ilifanyika siku ya Jumanne mjini Tehran, chini ya uenyekiti wa Ali Bagheri, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran anayeshughulikia masuala ya kisiasa na Ettore Plato, Katibu Mkuu katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Italia.
-
Mauaji mapya ya ufyatuaji risasi huko Marekani na radiamali ya pupa ya Biden
May 26, 2022 02:10Katika kisa kingine cha ufyatuaji risasi dhidi ya umati nchini Marekani ambacho kimepelekea kuuawa wanafunzi wengi ya shule ya msingi, Rais Joe Biden wa nchi hiyo kama alivyofanya katika siku za nyuma, ametoa radiamali ya pupa na isiyo ya busara katika uwanja huo.