-
Viongozi wa Marekani wanyoosheana vidole vya lawama kuhusu kufedheheshwa nchi hiyo huko Afghanistan
Aug 20, 2021 04:49Kufuatia kuingia tena madarakani huko Afghanistan kundi la Taliban, ambayo ni ishara ya wazi ya kushindwa vibaya kijeshi nchi hiyo ya Magharibi, Rais Joe Biden amekososlewa vikali kuhusiana na siasa zake za kuondoa askari wa nchi hiyo katika ardhi ya Afghanistan, ambapo sasa vyombo tofauti vya intelijensia na usalama vya Washington vinarushiana lawama kuhusu kadhia hiyo.
-
Al Houthi: Saudi Arabia ijifunze kutokana na kushindwa Marekani huko Afghanistan
Aug 19, 2021 19:36Mjumbe wa ngazi ya juu wa Baraza la Kisiasa la harakati ya Ansarullah ya Yemen amesema kuwa utawala wa kifalme wa Saudi Arabia unapaswa kujifunza na kupata ibra kutokana na tajiriba ya kushindwa na kufeli Marekani huko Afghanistan.
-
Ripoti mpya kuhusu matokeo ya vita vya miaka 20 vya Marekani huko Afghanistan
Aug 19, 2021 19:34Taasisi ya Watson Institute for International and Public Affairs katika Chuo Kikuu cha Brown imetangaza katika ripoti yake mpya kwamba, Marekani imetumia dola trilioni 2.26 katika vita vyake vya miaka 20 huko Afghanistan ambavyo vilianza msimu wa mapukutiko wa mwaka 2001.
-
New York Times lafichua: CIA ilimtahadharisha Biden kuhusu mgogoro utakaozuka Afghanistan
Aug 18, 2021 22:48Gazeti la New York Times limefichua kuwa, kabla wanajeshi wa Marekani hawajaondoka Afghanistan, Shirika la Ujasusi la Marekani CIA lilikuwa limeshamtahadharisha rais wa nchi hiyo Joe Biden kuhusu mgogoro utakaozuka ndani ya Afghanistan.
-
Facebook yatakiwa kufuta matangazo ya AIPAC yanayoeneza chuki dhidi ya Waislamu
Aug 15, 2021 22:08Mtandao wa kijamii wa Facebook uko chini ya shinikizo yanayoutaka kuondoa matangazo yanayohujumu Uislamu na Waislamu dhidi ya mwakilishi Muislamu wa Kongesi ya Marekani Ilhan Omar, ambayo vikundi vya wanasheria vinasema yanahatarisha maisha ya mbunge huyo wa Minnesota.
-
Johnson akosoa uamuzi wa Marekani kuhusu Afghanistan
Aug 15, 2021 05:31Sambamba na kundi la Taliban kuendelea kuteka maeneo zaidi huko Afghanistan na kuongezeka wasiwasi kuhusu mustakbali wa nchi hiyo, Boris Johnson, Waziri Mkuu wa Uingereza alisema Ijumaa kwamba hali ya Afghanistan ni mbaya mno na kwamba inatokana na uamuzi wa Rais Joe Biden wa kuondoa askari wa Marekani nchini humo.
-
Poland yakataa kulipa fidia kwa Marekani na Israel
Aug 14, 2021 21:54Waziri Mkuu wa Poland, Mateusz Morawiecki amepinga ukosoaji uliolenga hatua ya Bunge la nchi hiyo ya kupasisha sheria mbili zinazohusiana na umiliki wa vyombo vya habari na Holocaust na kusema kuwa, hakuna uwezekano wa kuruhusu utawala wa Kizayuni wa Israel kumiliki vyombo vya habari vya Poland.
-
Billy Prempeh: Wamarekani weusi wanabaguliwa katika utoaji wa chanjo ya corona
Aug 14, 2021 08:20Mgombea wa chama cha Republican katika jimbo la New Jersy katika uchaguzi wa Kongresi ya Marekani amekosoa ubaguzi unaoshuhudiwa nchini humo dhidi ya Wamarekani weusi katika utoaji wa chanjo ya corona.
-
Umoja wa Mataifa wakosoa vikwazo vya upande mmoja
Aug 13, 2021 04:35Wataalamu huru wa Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa wamesema katika taarifa iliyosambazwa Jumatano kwamba vikwazo vya upande mmoja vinavyotekelezwa kimataifa na baadhi ya nchi vimewapokonya watu wengi ulimwenguni haki yao ya kujistawisha kimaendeleo.
-
Biden azidi kupungukiwa na fahamu, mara hii amepotea njia ya kuelekea ofisini kwake White House!
Aug 12, 2021 21:55Rais Joe Biden wa Marekani ameendelea kuonyesha kuwa, mbali na kuboronga katika uzungumzaji, anazidi kupungukiwa na fahamu pia baada ya kupotea njia ya kuelekea ofisini kwake katika Ikulu ya White House.