Feb 23, 2022 11:47
Mkutano wa Sita wa Wakuu wa Jumuiya ya Nchi Zinazouza Nje Gesi Asilia (GECF) ulianza rasmi Jumanne wiki hii ukihudhuriwa na Rais Sayyid Ebrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, wakuu na wawakilishi wa nchi wanachama wa jumuiya hiyo. Mkutano huo ilifunguliwa kwa hotuba ya Amir wa Qatar, Sheikh Tamim bin Hamad al-Thani kwa kauli mbiu ya "Usalama wa Nishati Duniani".