-
Kuafiki bunge la Misri jeshi la nchi hiyo lipelekwe Libya
Jul 21, 2020 22:03Wakati mgogoro na mapigano yangali yanaendelea nchini Libya, uingiliaji wa madola ajinabi katika masuala ya ndani ya nchi hiyo umezidi kuongezeka. Katika mwendelezo wa uingiliaji huo, siku ya Jumatatu bunge la Misri lilitoa idhini kwa rais Abdel Fattah el Sisi ya kutuma askari na kujiingiza kijeshi nchini Libya itapolazimu kufanya hivyo; na vilevile likaafikiana na mpango wa kutumwa vikosi vya ulinzi vya nchi hiyo nje ya nchi kwa ajili ya shughuli za kijeshi.
-
Uturuki na Misri katika ncha ya kutumbukia kwenye vita nchini Libya
Jul 19, 2020 02:09Kushadidi hitilafu za Uturuki na Misri kuhusiana na kadhia ya Libya kumezifanya nchi hizo zipigane makumbo katika Umoja wa Mataifa na taasisi nyingine za kimataifa.
-
Misri yavunja rekodi Afrika, zaidi ya wagonjwa 700 wa corona wapatikana siku moja
Jul 18, 2020 03:35Wizara ya Afya ya Misri imetangaza kuwa, zaidi ya wagonjwa 700 wa COVID-19 wamegunduliwa nchini humo katika kipindi cha siku moja.
-
Erdoğan: Tutaiunga mkono Serikali ya Mwafaka wa Kitaifa ya Libya kukabiliana na Misri
Jul 18, 2020 03:29Rais Recep Tayyip Erdoğan wa Uturuki amesema kuwa nchi yake itaiunga mkono Serikali ya Mwafaka wa Kitaifa ya Libya kukabiliana na Misri na kamwe haitowaacha mkono wananchi wa Libya.
-
Serikali ya Mwafaka wa Kitaifa Libya yalaani vitisho vya al Sisi vya kuivamia nchi hiyo
Jul 17, 2020 22:01Serikali ya Mwafaka wa Kitaifa ya Libya (GNA) imelaani vikali matamshi yaliyotolewa na Rais Abdel Fattah al Sisi wa Misri aliyetishia kuvamia ardhi ya Libya.
-
Misri yaionya Uturuki, yasema operesheni dhidi ya mji wa Sirte huko Libya ni hatua hatari sana
Jul 14, 2020 06:22Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Misfri amekosoa vikali matamshi yaliyotolewa na mwenzake wa Uturuki kwamba Ankara inajitayarisha kushiriki katika operesheni ya kijeshi katika mji wa Sirte huko Libya na kusema matamshi hayo kuwa ni hatari kubwa.
-
Mgogoro wa bwawa la al Nahdha ungali unazitesa Misri, Sudan na Ethiopia
Jul 13, 2020 03:03Wizara ya Umwagiliaji Maji ya Misri imetangaza habari ya kuendelea mgogoro baina ya nchi hiyo na Sudan na Ethiopia katika siku ya kumi ya mazungumzo ya nchi hizo tatu kuhusu bwawa la al Nahdha.
-
Misri yataka nchi za dunia ziache kupeleka magaidi maeneo ya machafuko
Jul 13, 2020 02:44Mwakilishi wa kudumu wa Misri katika Umoja wa Mataifa ametoa mwito kwa viongozi wa baadhi ya nchi waache kupeleka magaidi katika maeneo ya machafuko hasa wakati huu wa kuenea maambukizi ya kirusi cha corona.
-
Mahakama Misri yathibitisha hukumu ya kifungo cha maisha jela alichohukumiwa kiongozi wa Ikhwanul Muslimin
Jul 09, 2020 21:56Mahakama Kuu ya Misri imethibitisha hukumu ya kifungo cha maisha jela aliyopewa kiongozi wa harakati ya Kiislamu ya Ikhwanul Muslimin Muhammad Badie pamoja na wenzake watano.
-
Wasiwasi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu kuongezeka uingiliaji wa kigeni nchini Libya
Jul 09, 2020 21:54Vita vya wenyewe kwa wenyewe huko Libya vimechukua sura mpya na tata na hasa kufuatia uamuzi wa wapiganaji wanaojiita Jeshi la Kitaifa la Libya linaloongozwa na jenerali muasi Khalifa Haftar wa kuanzisha hujuma ya kuuteka mji mkuu wa nchi hiyo Tripoli, mnamo mwezi Aprili 2019 na uingiliaji wa nchi za kigeni kwa ajili ya kuziunga mkono pande hasimu katika mgogoro huo.