-
Libya yahamishia nchini Misri wahamiaji haramu 95
Oct 17, 2019 23:55Serikali ya Libya imewahamishia nchini Misri makumi ya wahamiaji haramu wanaodaiwa kuwa na magonjwa ya kuambukiza.
-
Azma ya Ethiopia, Misri kuhusu mazungumzo ya ujenzi wa bwawa la Mto Nile
Oct 12, 2019 08:38Rais wa Misri Abdel-Fatah al-Sisi na waziri mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed wamesisitiza umuhimu wa kuondoa vizuizi vyote vinavyokabili mazungumzo ya pande tatu juu ya Bwawa la GERD linalojengwa na Ethiopia kwenye Mto Nile.
-
Zaidi ya walimu 1000 wafutwa kazi nchini Misri kwa tuhuma za kuwa wafuasi wa Ikhwanul Muslimin
Oct 08, 2019 23:03Wizara ya Elimu ya Misri imetoa amri ya kuwafuta kazi walimu 1070 kwa tuhuma za kuwa wanachama wa kundi la Ikhwanul Muslimin. uamuzi huo umetolewa kufuatia maandamano ya hivi karibuni nchini humo dhidi ya serikali ya Abdel Fattah al Sisi.
-
El Sisi 'apigwa mnada' kwa nusu pauni katika mitandao ya kijamii, serikali ya Misri yaja juu
Oct 07, 2019 15:33Mwanaharakati na mpinzani wa Rais Abdel Fattah el Sisi wa Misri ameanzisha kampeni ya Hashtagi katika mtandao wa kijamii wa Twitter ya kumpiga mnada kiongozi huyo kwa thamani haba na duni.
-
Licha ya kukumbwa na kashfa za wizi, mauaji na maadili maovu, kasisi mmoja Misri amwita Abdel Fattah el Sisi kuwa ni Nabii wa Mungu
Oct 07, 2019 04:25Kasisi wa kanisa moja nchini Misri, mfuasi wa rais wa nchi hiyo, Abdel Fattah el Sisi ametoa matamshi ya ajabu ya kumsifu kupindukia rais huyo licha ya kwamba ana kashfa nyingi za wizi, mauaji ya watu na maadili maovu.
-
Misri: Mazungumzo yetu na Ethiopia kuhusu bwawa la al-Nahdhah yamevunjika
Oct 06, 2019 04:43Serikali ya Misri imesema mazungumzo mapya kati ya nchi hiyo na Ethiopia kuhusu bwawa la al-Nahdhah linalojengwa na Addis Ababa yamegonga mwamba.
-
Maelfu watiwa nguvuni Misri katika maandamano yanayomtaka al Sisi ang'atuke
Oct 04, 2019 23:09Kamisheni ya Haki na Uhuru ya Misri imetangaza kuwa, askari usalama wa nchi hiyo wamewatia nguvuni raia zaidi ya elfu 3 katika maandamano ya wiki mbili za hivi karibuni dhidi ya Rais Abdel Fattah al Sisi wa nchi huyo.
-
Spika wa Bunge Misri amfananisha Rais wa nchi hiyo na Adolf Hitler
Oct 03, 2019 04:27Spika wa Bunge la Misri amemfananisha Rais Abdel Fattah al Sisi wa nchi hiyo na dikteta wa zamani wa Ujerumani Adolf Hitler.
-
Amnesty International: Misri ni gereza kubwa la wakosoaji wa serikali
Sep 30, 2019 04:41Shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limekosoa vikali ukandamizaji na kamatakamata dhidi ya waandamanaji nchini Misri na kusisitiza kuwa nchi hiyo imegeuzwa kuwa gereza kubwa la wakosoaji.
-
Usalama waimarishwa Misri kukabiliana na maandamano dhidi ya Rais Abdul-Fattah al-Sisi
Sep 29, 2019 09:00Usalama umeimarishwa kote nchini Misri ili kukabiliana na maandamano ya wananchi dhidi ya Rais wa nchi hiyo Abdul-Fattah al-Sisi ambayo yameshadidi na kutishia uongozi wake.