-
Kuanza tena maandamano ya wananchi huko Misri
Sep 29, 2019 03:40Wananchi wa Misri kwa mara nyingine wamemiminika mitaani kulalamikia matatizo ya kisiasa, kiuchumi na kijamii wanayokabiliana nayo na kutaka kuondoka madarakani rais wa nchi hiyo Abdel Fattah al Sisi baada ya kupita miaka 8 ya vuguvufu la harakati ya wananchi wa Misri lililopelekea kung'olewa madarakani dikteta wa zamani wa nchi hiyo Hosni Mubarak.
-
Al Sarraj ataka kukomeshwa uingiliaji wa nchi ajinabi huko Libya
Sep 26, 2019 23:08Waziri Mkuu na Mkuu wa baraza la uongozi la serikali ya umoja wa kitaifa ya Libya ametaka kusitishwa uingiliaji wa Imarati, Misri na Ufaransa katika masuala ya ndani ya nchi yake.
-
Kuendelea maandamano nchini Misri, sambamba na uungaji mkono wa Trump kwa Abdul-Fattah al-Sisi
Sep 26, 2019 07:15Katika hali ambayo, Rais Donald Trump wa Marekani alimtaja Rais Abdul-Fattah al-Sisi wa Misri walipokutana mjini New York makao makuu ya Umoja wa Mataifa kuwa, 'Kiongozi Mkubwa', maandamano dhidi ya serikali ya Cairo yameendelea kushuhudiwa katika miji mbalimbali ya nchi hiyo ya Kiarabu.
-
Wanachama 6 wa Ikhwanul Muslimin wauawa nchini Misri
Sep 25, 2019 04:16Wizara ya Mambo ya Ndani ya Misri imetangaza kuwa, polisi wa nchi hiyo wamewapiga risasi na kuwaua wanachama sita wa Ikhwanul Muslim katika mapigano yaliyotokea baina ya pande hizo mbili.
-
Waandamanaji zaidi ya 650 watiwa mbaroni Misri
Sep 23, 2019 09:03Vyombo vya sheria vya Misri vimewatia mbaroni wafanya maandamano zaidi ya 650. Watu hao walikuwa wakiandamana dhidi ya serikali ya Rais Abdel Fattah al Sisi.
-
Wamisri wafanya maandamano dhidi ya utawala wa Rais Sisi
Sep 21, 2019 02:44Wananchi wa Misri wamefanya maandamano dhidi ya Rais Abdel Fattah al-Sisi wa nchi hiyo.
-
Afisa wa zamani wa jeshi la Misri atishia kufichua ufuska wa Rais al Sisi
Sep 20, 2019 02:54Afisa wa zamani wa jeshi la Misri amesema kuwa anazo nyaraka zinazohusiana na ufuska na utovu wa maadili wa rais wa nchi hiyo katika masuala ya ngono.
-
Kadhaa wauawa katika makabaliano baina ya askari wa Misri na magaidi, Sinai
Sep 15, 2019 02:46Vyombo vya usalama vya Misri vimetangaza habari ya kuuawa watu kadhaa katika makabiliano baina ya wanajeshi wa serikali ya nchi hiyo na wanamgambo huko kaskazini mwa mkoa wa Sinai.
-
Trump amuita Rais Sisi wa Misri kuwa dikteta
Sep 14, 2019 07:05Rais Donald Trump wa Marekani ameripotiwa kumtaja Rais Abdul Fattah al-Sisi kuwa dikteta.
-
Misri yataka kuondolewa vikwazo vya Marekani dhidi ya Sudan
Sep 10, 2019 02:49Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri ametaka kuondolewa vikwazo vya Marekani dhidi ya Sudan, akisisitiza kuwa serikali mpya ya kiraia ya Khartoum inahitaji uungaji mkono wa jamii ya kimataifa na sio kuendelea kuwekewa vikwazo na kutengwa.