Al Sarraj ataka kukomeshwa uingiliaji wa nchi ajinabi huko Libya
(last modified Fri, 27 Sep 2019 02:38:56 GMT )
Sep 27, 2019 02:38 UTC
  • Al Sarraj ataka kukomeshwa uingiliaji wa nchi ajinabi huko Libya

Waziri Mkuu na Mkuu wa baraza la uongozi la serikali ya umoja wa kitaifa ya Libya ametaka kusitishwa uingiliaji wa Imarati, Misri na Ufaransa katika masuala ya ndani ya nchi yake.

Fayiz al Sarraj amelaani uingiliaji wa nchi ajinabi huko Lbya na kumtaja Jenerali Khalifa Haftar kuwa ni mtenda jinai mwenye kiu ya damu. Waziri Mkuu wa Libya ameyasema hayo akihutubia kikao cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa huko New York.  

Al Sarraj amelitaja jina la Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati), Ufatansa na Misri na kueleza kuwa: Inashangaza kuona nchi nyingine zinaendelea kuingilia masuala ya Libya na kumuunga mkono moja kwa moja Haftar ambaye ni mtenda jinai za kivita. 

Waziri Mkuu wa serikali ya umoja wa kitaifa ya Libya ameeleza kusikitishwa  na hali ya mgogoro inayoikabili Libya kutokana na uingiliaji hasi wa nchi ajinabi na kueleza kuwa Imarati yenyewe imejipa kibali cha kuwa chombo cha upashaji habari cha wanamgambo wa Khalifa Haftar; huku Misri nayo eti ikitaka kuipa somo Libya. 

Jenerali Khalifa Haftar 
 

Wanamgambo hao wanaojiita jeshi la kitaifa la Libya wanaoongozwa na Khalifa Haftar Aprili Nne mwaka huu walianzisha mashambulizi kwa lengo la kuudhibiti mji mkuu Tripoli hata hivyo hadi kufikia sasa wameshindwa kutimiza lengo lao hilo.  

Tags