Kamal Kharrazi: Uungaji mkono wa EU kwa UAE ni uadui wa wazi dhidi ya Iran
(last modified 2024-10-19T03:04:43+00:00 )
Oct 19, 2024 03:04 UTC
  • Kamal Kharrazi: Uungaji mkono wa EU kwa UAE ni uadui wa wazi dhidi ya Iran

Mkuu wa Baraza la Kistratejia la Uhusiano wa Nje la Iran amekosoa uingiliaji kati wa Umoja wa Ulaya (EU) kwa malengo yasiyofaa na kuunga mkono madai ya Imarati kuhusu visiwa vitatu vya Iran, na amewatahadharisha viongozi wa Imarati kwamba waache uadui wao na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Visiwa vitatu vya Bu-Musa, Tombu Kubwa na Tombu Ndogo viko katika Ghuba ya Uajemi na karibu na Lango Bahari la Hormuz; ambapo kwa mujibu wa nyaraka za historia za kuaminika, visiwa hivyo vilikuwa chini ya utawala wa Iran katika zama za Achaemenid na ni sehemu isiyoweza kutenganishwa ya ardhi ya Iran. 

Majuzi nchi za Umoja wa Ulaya na Baraza la Ushirikiano la nchi za pambizoni mwa Ghuba ya Uajemi katika kipengee cha mwisho ya taarifa yao ya pamoja, zilikariri madai yasiyo na msingi na ya huko nyuma kuhusu visiwa hivyo vitatu inavyomilikiwa na Iran. 

Sayyid Kamal Kharrazi ametoa taarifa na kuweka wazi malengo ya Umoja wa Ulaya ya kuunga mkono madai ya Imarati kuhusu visiwa vitatu vya Iran na kuwatahadharisha viongozi wa Imarati kuwa waache kuifanyia uadui Iran kuhusu suala la umoja wa ardhi yake. 

Mwanadiplomasia huyo wa ngazi za juu wa Iran pia ametaja sababu ya misimamo ya kiuadui ya Ulaya, ikiwa ni pamoja na kuyawekea vikwazo makampuni ya ndege ya Iran au katika taarifa yao ya hivi karibuni, kuwa ni uungaji mkono wa Jamhuri ya Kiislamu kwa Muqawama na mapambano ya ukombozi wa Palestina na uungaji mkono wa Ulaya kwa utawala ghasibu wa Israel. Amesema nchi hizo za Magharibi zinakabilina na Iran kwa kutuma silaha za maangamizi makubwa na misaada ya kifedha kwa utawala huo katili na mfyonza damu.

Mkuu wa Baraza la Kistratijia la Mahusiano ya Kigeni la Iran amekumbusha kwamba, ushahidi na nyaraka zinazohusiana na milki ya visiwa hivyo vitatu vya Iran ni zina nguvu na ziko wazi kiasi kwamba, taarifa kama hizo ziwezi kuathiri msimamo thabiti wa Tehran kwamba visiwa hivyo ni mali ya Iran, na nchi ya Iran. uamuzi wa majeshi ya Jamhuri ya Kiislamu katika Haileti ulinzi wa uadilifu wa eneo la Iran.

Amesisitiza kuwa, taifa hiyo haiwezi kuathiri azma ya vikosi vya jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya kutetea ardhi ya Iran.

Tags