Kuwait yakanusha uvumi wa kuupelekea silaha utawala wa Kizayuni
(last modified 2024-10-22T03:22:59+00:00 )
Oct 22, 2024 03:22 UTC
  • Kuwait yakanusha uvumi wa kuupelekea silaha utawala wa Kizayuni

Makao Makuu ya jeshi la Kuwait yamekanusha uvumi kwamba inahamisha silaha kutoka kambi za kijeshi ndani ya nchi hiyo na kuupelekea utawala wa Kizayuni wa Israel.

Katika siku za karibuni, mitandao ya kijamii imeripoti kuwa kuna silaha zinazohamishwa kutoka kituo cha Ali al-Salem cha Kuwait na kupelekwa kambi ya Neftayim ya utawala wa Kizayuni kupitia njia ya anga.
 
Kwa mujibu wa ripoti ya IRNA Jumatatu, kufuatia kuenea kwa habari hiyo, makao makuu ya Jeshi la Kuwait yameeleza katika taarifa kwamba: chochote kilichotangazwa katika baadhi ya vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kuhusu uhamishaji wa silaha kutoka vituo vya jeshi la anga la Kuwait hakina ukweli na kinakanushwa.
 
Makao makuu ya Vikosi vya Ulinzi vya Kuwait yameongeza katika taarifa hii kwamba: safari za ndege za kijeshi zinafanyika kulingana na ratiba zilizokuwa zimepangwa tokea hapo awali na hufanyika kwa uratibu na udhibiti.
 
Kabla ya hapo, vyombo vya habari vya utawala wa Kizayuni viliripoti wasiwasi lilionao jeshi la utawala huo kutokana na kupungukiwa na akiba ya silaha na risasi.
Miito inatolewa ya kuuwekea vikwazo vya silaha utawala wa Kizayuni

Hayo yanaripotiwa wakati jeshi la Marekani, ambalo ni msaidizi na muungaji mkono mkuu wa Israel, lina vituo vinne vya kijeshi nchini Kuwait, ambavyo ni Kituo cha Anga cha Ali Al Salem, Kituo cha Anga cha Arifjan, Kituo cha Anga cha Ahmed Al Jaber na Kituo cha Anga cha Ufalme wa Kuwait.

 
Tangu tarehe 7 Oktoba 2023, utawala wa Kizayuni ulianzisha vita angamizi dhidi ya wakazi wa Ukanda wa Ghaza na matokeo yake, ambavyo mbali na kusababisha uharibifu mkubwa na njaa ya kutisha, vimeua shahhidi zaidi ya watu elfu 42 na kujeruhi makumi ya maelfu ya wengine. 
 
Mbali na kuidharau jamii ya kimataifa, kupuuza maazimio ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ya kusitisha mara moja vita na kutojali maagizo ya Mahakama ya Kimataifa ya Haki kuhusu ulazima wa kuzuia mauaji ya kimbari na kuboresha hali mbaya ya binadamu huko Ghaza, utawala bandia wa Israel ungali unaaendeleza jinai zake katika eneo hilo uliloliwekea mzingiro.../

 

Tags