Kwa silaha na uwezeshaji wa US, Israel imedhamiria kuwahamisha Wapalestina wote wa Ghaza
(last modified 2024-10-20T06:43:43+00:00 )
Oct 20, 2024 06:43 UTC
  • Kwa silaha na uwezeshaji wa US, Israel imedhamiria kuwahamisha Wapalestina wote wa Ghaza

Hassan Mneimneh, mchambuzi wa kisiasa wa Taasisi ya Mashariki ya Kati, ameiambia Al Jazeera kwamba ukatili unyama na unaofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel katika Ukanda wa Ghaza umewezeshwa na Marekani na usambazaji wake wa silaha kwa ajili ya kuendesha vita katika eneo hilo la Palestina.

Mneimneh amesema, inapofikia hatua hiyo, na kutokana na ukimya na ushiriki usio rasmi wa Marekani kwa njia ya utoaji silaha katika jinai zote zinazofanywa na Israel, haiwezekani kuepuka kauli kwamba bila shaka yoyote, Marekani ni mshirika ya jinai hizo.
 
Kwa mujibu wa mchambuzi huyo, kuzingirwa eneo la kaskazini ya Ghaza na kuwalenga kwa mabomu na makombora raia wanaokimbia kunaonekana kuwa ni jaribio la makusudi la Israel la kunyakua ardhi ya Palestina na "kuwafukuza Wapalestina kwa nguvu za kikatili".
Hali ya kutisha ya mashambulio ya kinyama ya Israel Ghaza

Mneimneh amesisitiza kwa kusema: "hali za kuogofya tunazoshuhudia" huko Ghaza "zimewezeshwa" na Marekani.

 
Mchambuzi huyo wa kisiasa wa Taasisi ya Mashariki ya Kati ameendelea kueleza: "tunashuhudia, kwa kweli, onyesho la kuogofya hapa. Na kwa mara nyingine tena, hatuwezi kutenganisha hilo na ukimya, kutojali, -ambako kidhahiri kunaonekana kama kutojali-, lakini kiuhalisia ni ushiriki wa mwezeshaji. Israel isingeweza kufanya hivyo kama utawala wa Marekani usingeiwezesha kufanya hivyo”.
 
Mneimneh amemalizia kwa kusema: "Israel inakifikia kile ambacho kwa ushahidi wa wazi ndilo lengo lake lisilo na shaka katika operesheni hii yote, nalo ni kutobakisha mtu yeyote katika ukanda wa Ghaza".../

 

Tags