Mtazamo wa Hamas wa kuendeleza mapambano dhidi ya utawala wa Kizayuni na ukombozi wa Palestina
(last modified 2024-10-22T02:25:21+00:00 )
Oct 22, 2024 02:25 UTC
  • Mtazamo wa Hamas wa kuendeleza mapambano dhidi ya utawala wa Kizayuni na ukombozi wa Palestina

Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina (Hamas) na makundi mengine ya Muqawama ya Palestina yanaendeleza mapambano dhidi ya utawala wa Kizayuni kwa shabaha ya kuikomboa Palestina.

Lengo kuu la Hamas ni kuendeleza mapambano dhidi ya utawala wa Kizayuni na ukombozi wa Palestina. Yakiwa bega kwa bega na Hamas, makundi mengine ya mapambano ya Palestina yanatambua kuwa mapambano ndiyo njia bora na yenye ufanisi zaidi ya kukabiliana na utawala wa Kizayuni kwa kuzingatia matokeo ya Oparesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa. Uzoefu wa matukio ya kieneo na mapambano dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel vinadhihirisha ukweli kwamba, kuendelezwa muqawama ndiyo stratijia muhimu na madhubuti zaidi ya kukabiliana na Wazayuni.

Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina "Hamas

Uratibu na ushirikiano wa makundi ya Muqawama katika vita vya Ukanda wa  Gaza uliuweka utawala wa Kizayuni katika hali ya kukata tamaa na viongozi wa Kizayuni wamelazimika kukiri kwamba hawana uwezo wa kukabiliana na mashambulizi ya Kambi ya Muqawama katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu na Israel. Licha ya Tel Aviv kusaidiwa na Marekani na nchi nyingine za Magharibi, Wazayyuni wamepata kipigo kisichoweza kufidiwa katika vita dhidi ya makundi ya Muqawama ya Palestina, na vituo vingi vya kijeshi, kiusalama na kijasusi vya utawala wa Kizayuni vimeshambuliwa katika ardhi hizo zinazokaliwa kwa mabavu.

Kwa upande mwingine, utawala wa Kizayuni unaendelea kufanya jinai na mauaji ya kimbari huko Gaza ili kuepuka kushindwa katika medani ya vita, na wakati huo huo unaendeleza oparesheni za kigaidi dhidi ya  viongozi wa Muqawama. Hata hivyo, ugaidi uliopangwa na mauaji ya kimbari ya utawala wa Kizayuni dhidi ya Wapalestina  yameshindwa kuzuia oparesheni za makundi ya Muqawama ya  Palestina.

Mbali na operesheni za Muqawama na utekelezwaji wa mbinu mbalimbali za kijeshi, moyo wa kupenda kufa shahidi na mapambano pia umeimarisha sana umoja wa makundi ya Muqawama ya Palestina, na hatua za kigaidi za utawala wa Kizayuni dhidi ya viongozi wa Muqawama zinazidisha azma ya makundi haya ya kupambana kwa nguvu zote na kusimama kidete katika medani ya vita. Ismail Haniyeh na Yayha Sinwar, walikuwa miongoni mwa viongozi wa harakati ya Hamas waliouawa shahidi katika hujuma za kigaidi na jinai za kinyama za Israel, lakini si tu kwamba mapambano yamesimama, bali yanaendelea dhidi ya Wazayuni kwa mshikamano na  nguvu zaidi kuliko hapo awali.

Matukio ya wiki za hivi karibuni huko Ukanda wa Gaza yamefichua kuwa, ugaidi uliopangwa wa utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya viongozi wa Muqawama sio tu kwamba hayakutia dosari yoyote katika mapambano ya makundi ya Muqawama ya Palestina, bali pia yamezidisha ari na moyo wa mapambano. 

Khaled Mashal, mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Hamas nje ya nchi, amesisitiza kwamba licha ya kuuawa shahidi Yahya Sinwar, Hamas inashikimana barabara na chaguo la Muqawama hadi ukombozi kamili wa Palestina utakapopatikana. Katika hotuba ya kuenzi kumbukumbu ya Shahidi Yahya Sinwar, Mash'al  pia amesema,  Harakati hii daima imekuwa ikitsabilia viongozi wake katika njia ya kufa shahidi, fahari, ukombozi wa ardhi na uhuru wa Palestina kutokana kkwenye uvamizi wa utawala katili wa Israel.

Khaled Mash'al Afisa wa ngazi ya juu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina