Iran: Tumeshaainisha maeneo yote ya Israel yanayopaswa kupigwa na silaha zetu
(last modified 2024-10-20T11:19:54+00:00 )
Oct 20, 2024 11:19 UTC
  • Iran: Tumeshaainisha maeneo yote ya Israel yanayopaswa kupigwa na silaha zetu

Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, shambulio lolote litakalofanywa na utawala wa Kizayuni dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu litajibiwa viikali na kwamba, maeneo yote ya Israel yanayopaswa kupigwa kwa silaha za Iran, yameshaainishwa.

Kwa mujibu wa shirika la habari la FARS, Sayyid Abbas Araghchi amesema hayo katika mahojiano aliyofanyiwa na televisheni ya NTV ya Uturuki na kusema kuhusu kuuawa shahidi kiongozi wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS, Yahya Sinwar kwamba, harakati hiyo ya Kiislamu kamwe hazitosimama bali kitakachokuwepo ni kuongezeka tu nguvu na mori wa vijana wa Palestina hadi utakapopatikana ukombozi wa ardhi zote za taifa hilo. 

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ameongeza kuwa, utawala wa Kizayuni hauwezi kuendelea na jinai zake wala kuwepo katika uso wa dunia bila ya msaada wa pande zote wa Marekani. Jinai zote zinazofanywa na Israel huko Palestina na Lebanon zinafanyika kwa uungaji mkono na msaada kamili wa Marekani. Silaha zote zinazotumiwa na Israel kufanya jinai zinatoka kwa Marekani. 

Sayyid Abbas Araghchi, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran

 

Vile vile ameonya kuhusu hatari ya kuenea vita hadi katika nchi nyingine za Ghuba ya Uajemi lakini wakati huo huo amesema kwamba, njia za kidiplomasia bado zipo na haiwezekani kila kitu kukikabidhi katika maamumizi ya mtu mmoja ndani ya utawala wa Kizayuni.

Pia amesema, chokochoko zozote zitakazofanywa na Israel dhidi ya Iran zitapata majibu makali na iwapo utawala wa Kizayuni utashambulia taasisi za nyuklia za Iran, Jamhuri ya Kiislamu nayo itasambaratisha taasisi za nyuklia za Israel.