Wazayuni wenye misimamo mikali wavamia tena msikiti wa al-Aqswa
(last modified 2024-10-22T02:23:36+00:00 )
Oct 22, 2024 02:23 UTC
  • Wazayuni wenye misimamo mikali wavamia tena msikiti wa al-Aqswa

Walowezi wa Kizayuni wenye misimamo ya kufurutu ada wamevamia tena msikiti mtakatifu wa wa Al-Aqsa kwa siku ya pili mtawalia na kufanya vitendo vya kichochezi dhidi ya kibla hicho cha kwanza cha Waislamu.

Habari kutoka Palestina zinasema kuwa, jana kama ilivyokuuwa sikuu ya Jumapili, Jumatatu ya jana pia zaidi ya walowezo 500 wa Kizayuni walivamia msikiti wa al-Aqswa ambapo sambamba na kupiga nara dhidi ya Wapalestina walifanya vitendo vya kichochezi katika eneo hilo takatifu.

Msikiti wa al-Aqswa unajulikana kuwa nembo kuu ya utambulisho wa Kiislamu na Kipalestina wa eneo takatifu la Quds na utawala wa Israel unajaribu kuharibu utambulisho huo, lakini kusimama imara na kuwa macho wananchi wa Palestina kumeufedhehesha utawala huo wa Kizayuni na kupelekea njama zake kushindwa.

Walowezi wengi wa Kizayuni wenye misimamo mikali mara kwa mara wamekuwa wakivamia msikiti wa al-Aqswa kibla cha kwanza cha Waislamu na kufanya vitendo vya kichochezi huku wakiwa wanapatiwa ulinzi na vikosi vya usalama vya utawala haramu wa Israel.

 

Vitendo vya hujuma za walowezi wa Kizayuni dhidi ya msikiti wa al-Aqswa vimekithiri zaidi baada ya kuingia madarakani serikali yenye misimamo mikali ya Benjamin Netanyahu ambayo imekuwa ikionyesha chuki za wazi wazi dhidi ya Wapalestina na maeneo yao matakatifu.

Vitendo vya kuyavunjia heshima matukufu ya Kiislamu huko Palestina vinafanyika katika hali ambayo, viongozi wa nchi za Kiarabu na jamii ya kimataifa wameendelea kunyamaza kimya na kutochukua hatua zozote za maana za kukabiliana na vitendo hivyo vinavyokinzana na utu na ubinadamu.

Tags