Wanajeshi 15 wa Kizayuni wajeruhiwa katika mashambulizi ya makombora ya Hizbullah
(last modified 2024-10-21T11:24:34+00:00 )
Oct 21, 2024 11:24 UTC
  • Wanajeshi 15 wa Kizayuni wajeruhiwa katika mashambulizi ya makombora ya Hizbullah

Harakati ya Mapambano ya Hizbullah ya Lebanon imeyashambulia kwa makombra maeneo mbalimbali ya utawala wa Kizayuni na kuwajeruhi wanajeshi 15 wa utawala huo.

Shirika la habari la IRNA limeripoti kuwa, makombora hayo yaliyovurumishwa na Hizbullah kuelekea maeneo yanayokaliwa kwa mabavu (Israel) yamesababisha kusikika ving'ora vya hatari katika maeneo ya Manareh na Mergliot huko Esba al-Jalil. 

Hizbullah imevurumisha zaidi ya makombora 25 katika eneo la "Karmeel" huko al Jalil ambapo ving'ora vya hatari vimesikika katika eneo hilo. 

Harakati ya Hizbullah ya Lebanon imerusha pia makombora upande wa kaskazini mwa Golan inayokaliwa kwa mabavu. Baadhi ya duru pia zimeripoti kuhusu kupenya ndege kadhaa zisizo na rubani katika eneo la "Niyot Mordechai" huko al Jalil.

Wakati huo huo, hospitali ya Kizayuni ya Zif katika eneo la Safed imetangaza kuwa wanajeshi 15 wa Israel walihamishiwa katika hospitali hiyo kutoka katika maeneo ya vita yanayopakana na Lebanon kufuatia mashambulizi  ya jana usiku ya Hizbullah.

Tags