Hizbullah yazindua mtambo mpya wa makombora
(last modified 2024-10-20T02:43:26+00:00 )
Oct 20, 2024 02:43 UTC

Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Lebanon, Hizbullah imezindua mtambo wake wa maroketi wa M80 maalumu kwa kurushia maroketi ya kushambulia adui kutoka ardhini hadi ardhini.

Kwa mujibu wa Shirika la Utangazaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran IRIB, vyombo vya habari za vita vya Muqawama wa Kiislamu vya Lebanon vimeonyesha mkanda wa video na kutangaza kuwa Hizbullah imeanza kutumia kwa mara ya kwanza mtambo wa maroketi wa M80.
 
Kwa mujibu wa video hiyo iliyoonyeshwa na Hizbullah, mtambo huo wa maroketi unafika masafa yenye umbali wa kilomita 3.3 na maroketi yake yanashambulia kimbinu na kitaktiki kutoka ardhini hadi ardhini.
 
Vyombo vya habari za vita vya Muqawama wa Kiislamu wa Lebanon vimeonyesha pia video ya utekelezaji wa operesheni iliyolenga kituo cha wanamaji wa jeshi la utawala wa Kizayuni cha Ras al-Naqourah.
 
Wiki iliyopita, harakati ya Hizbullah ya Lebanon ilizindua pia makombora ya balestiki yenye shabaha kali ya Qadir 2 na Nasr 1.../

 

Tags