Ripota wa UN: Mauaji ya kimbari ya Israel dhidi ya Ukanda wa Gaza ni "aibu ya pamoja ya karne"
(last modified 2024-10-21T11:35:10+00:00 )
Oct 21, 2024 11:35 UTC
  • Ripota wa UN: Mauaji ya kimbari ya Israel dhidi ya Ukanda wa Gaza ni

Ripota Maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya haki za binadamu katika maeneo ya Palestina yanayokaliwa kwa mabavu ameyataja mauaji ya kimbari yanayoendelea kufanywa na Israel katika Ukanda wa Gaza kuwa ni "aibu ya pamoja ya karne" huku jamii ya kimataifa ikishindwa kulinda haki za Wapalestina.

Bi Francesca Albanese ameeleza haya katika ujumbe wake aliotuma katika mtandao wa kijamii wa X ikiwa umepita zaidi ya mwaka mmoja wa mauaji ya kimbari ya Israel dhidi ya wakazi wa Gaza ambayo yameua maelfu ya watu wasio na hatia na kusababisha karibu jamii nzima ya ukanda huo ulio chini ya mzingiro kuwa wakimbizi.  

"Huko Gaza aibu ya pamoja ya karne hii inaendelea bila kusitishwa kinyume na kila kanuni za maadili na sheria zote za kimataifa," amesema Ripota Maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya haki za binadamu katika maeneo ya Palestina yanayokaliwa kwa mabavu.

Francesca Albanese

Amesema Wapalestina wamechoshwa na mashambulizi ya mara kwa mara dhidi yao na kwamba mauaji ya kiholela, kuhamishwa watu wengi kwa mabavu na vitendo vingine viovu vya unyanyasaji ambavyo vinatekelezwa na wanajeshi wa utawala vamizi dhidi ya raia hao katika Ukanda wa Gaza yote hayo ni ushuhuda wa aibu mkabala wa kimya na kushindwa kuchukua hatua jamii ya kimataifa ili kulinda haki za kimsingi za binadamu. 

Utawala ghasibu wa Tel Aviv hadi sasa umewaua shahidi Wapalestina wasiopungua 42,603, wengi wao wakiwa wanawake na watoto, na kujeruhi wengine 99,795. Takwimu hizi ni kwa mujibu wa Wizara ya Afya ya Gaza.

 

Tags