Rais wa Afrika Kusini aitaka dunia kuishinikiza Israel kusitisha mashambulizi huko Gaza, Lebanon
(last modified 2024-10-15T02:45:04+00:00 )
Oct 15, 2024 02:45 UTC
  • Rais wa Afrika Kusini aitaka dunia kuishinikiza Israel kusitisha mashambulizi huko Gaza, Lebanon

Rais wa Afrika Kusini jana aliwataka vingozi wa nchi mbalimbali duniani kuushinikiza utawala wa Israel ili kusitisha mashambulizi yake katika Ukanda wa Gaza na Lebanon.

"Tunatoa wito wa kusitishwa mauaji na mashambulizi mara moja huko Gaza. Kuachiliwa kwa mateka na pia kuhakikisha misaada ya kibinadamu inawafikia watu", amesema Rais Cyril Ramaphosa akiwahutubia wafuasi wa chama tawala ANC mjini Johannesburg akiadhimisha siku 100 za kuwa kwake madarakani.

Chama cha ANC ambacho kimeiongoza Afrika Kusini tangu mwaka 1994 kilipoteza viti vingi vya uwakilishi bungeni katika uchaguzi wa taifa wa mwezi Mei mwaka huu na hivyo kulazimika kuunda serikali ya muungano. 

Ramaphosa ameeleza kuwa siku kadhaa zijazo serikali yake itawasilisha kesi yake kamili katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki ya (ICJ) katika kuwaunga mkono wananchi wa Palestina dhidi ya mauaji ya kimbari yanayoendelea kufanywa dhidi ya wananchi wa Palestina khususan huko Gaza. 

Israel inatekeleza mauaji ya kimbari dhidi ya wakazi wa Ukanda wa Gaza 

Amesema serikali yake itahakikisha inaendelea kusaidia watu wa Palestina. 

Afrika Kusini iliwasilisha kesi yake katika mahakama hiyo ya mjini The Hague mwishoni mwa mwaka jana ikiituhumu Israel, ambayo inatekeleza mauaji ya kimbari na mahambulizi ya kinyama katika Ukanda wa Gaza tangu Oktoba mwaka jana, kwa kushindwa kutekeleza ahadi zake kwa mujibu wa Mkataba wa Mauaji ya Kimbari wa mwaka 1948.

 

Tags