Utafiti: 86% ya Wazayuni hawataki tena kuishi karibu na Gaza baada ya vipigo
(last modified 2024-10-07T02:19:36+00:00 )
Oct 07, 2024 02:19 UTC
  • Utafiti: 86% ya Wazayuni hawataki tena kuishi karibu na Gaza baada ya vipigo

Utafiti mpya wa maoni umefichua kuwa, asilimia 86 ya Waisraeli wanasema hawataishi tena katika vitongoji vya walowezi wa Kizayuni vilivyoko karibu na Ukanda wa Gaza baada ya kumalizika mgogoro huo mbaya zaidi wa kibinadamu uliosababishwa na chokochoko za Tel Aviv.

Utafiti huo wa maoni uliofanywa na shirika rasmi la utangazaji la Israel KAN kwa kuwashirikisha Wazayuni laki sita unaonyesha kuwa, ni asilimia 14 pekee ya Waisraeli wamesema wangelitafakari kuishi katika maeneo yanayopakana na Gaza.

Utafiti huo umeonyesha kuwa, asilimia 35 ya Waisraeli wanaamini kuwa, utawala huo umeshindwa vita na Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS huku asilimia 27 pekee wakisema "umeshinda". 

Baada ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kutoa vipigo vikali vya makombora dhidi ya maeneo hasasi ya utawala wa Kizayuni, wimbi la kuakhirishwa safari za ndege za kuingia na kutoka Israel nalo limevunja rekodi huku idadi ya walowezi wa Kizayuni walioamua kukimbia ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu ikiongezeka mno.

Hata kabla ya hapo pia, mashirika ya ndege ya kimataifa yalikuwa yamesimamisha au kupunguza safari zao za kuelekea Israel baada ya utawala wa Kizayuni kushadidisha mashambulio yake dhidi ya Lebanon ambayo yalipelekea pia kuuawa shahidi kidhulma, Sayyid Hassan Nasrullah, Katibu Mkuu wa Hizbullah.

Wimbi hilo lilivunja rekodi baada ya Iran kuyatwanga kwa makombora baadhi ya maeneo nyeti ya utawala wa Kizayuni katika operesheni ya ulipizaji kisasi ya Ahadi ya Kweli 2.

 

Tags