Rais wa Iran akosoa unafiki na undumakuwili wa Wamagharibi
(last modified 2024-10-21T02:55:08+00:00 )
Oct 21, 2024 02:55 UTC
  • Rais wa Iran akosoa unafiki na undumakuwili wa Wamagharibi

Rais wa Iran, Masoud Pezeshkian amekosoa vikali undumakuwili wa utawala haramu wa Israel na Marekani akisisitiza kuwa, Wamagharibi wakiongozwa na Tel Aviv na Washington wanaongoza kwa unafiki licha ya madai yao ya kupigania demokrasia, haki za binadamu na uhuru.

Akizungumza katika hafla ya kitaifa jana Jumapili, Dakta Pezeshkian alisema haingii akilini namna Israel inavyozungumzia maadili kama vile demokrasia na haki za binadamu, wakati ambapo utawala huo unatekeleza sera za kikatili.

Rais wa Iran amehoji kwa kuksema: "Ni dhamiri gani iliyoamka inayoweza kukubali kwamba Wazayuni wanazungumzia juu ya demokrasia, haki za binadamu na uhuru huku wanafanya vitendo vya kinyama zaidi?" 

Kadhalika Dakta Pezeshkian amekosoa vikali unafiki wa Marekani na washirika wake wa kikanda, huku akilaani ghasia na ugaidi ambao umekuwa ukifanywa katika eneo hili.

Rais wa Iran ameashiria mkakati mpana wa kuyumbisha utulivu katika eneo hili na kueleza kuwa, "Idadi ya watu waliouawa katika operesheni za kigaidi zinazofanywa na Marekani na genge lake katika eneo hili, hazilinganishwi na wengine." 

Licha ya shinikizo kubwa kutoka nje, Pezeshkian alisisitiza azimio la Iran la kushinda changamoto na kulijenga upya taifa.

"Wametuweka katika hali ambayo hatuwezi kuiendeleza Iran, lakini tumedhamiria kuijenga upya nchi," ameeleza Rais wa Iran na kusisitiza dhamira ya serikali yake ya ukuaji wa taifa licha ya uingiliaji wa nchi za nje.

Tags