Iran yalaani mauaji ya kinyama ya Israel Beit Lahiya
(last modified Wed, 30 Oct 2024 03:31:30 GMT )
Oct 30, 2024 03:31 UTC
  • Iran yalaani mauaji ya kinyama ya Israel Beit Lahiya

Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amelaani vikali jinai na hujuma ya umwagaji damu huko Bait Lahiya iliyofanywa na utawala haramu wa Israel.

Ismail Baqaei ametoa wito wa kuchukuliwa hatua madhubuti za kimataifa ili kukomesha jinai na kufanyika juhudi za kuwaadhibu viongozi wa utawala ghasibu wa Israel.Msemaji huyo wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema, kuendelea uvamizi wa maeneo ya makazi ya watu na mauaji ya umati ya watu wa Gaza ambayo yanaambatana na kuzingirwa kikamilifu Ukanda wa Gaza na kuzuia misaada ya kibinadamu ni mfano wa wazi wa jinai ya kivita na sehemu ya mpango wa kuliangamiza taifa la Palestina na kuwahamisha kwa nguvu kutoka katika ardhi yao.

Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran amesisitiza wajibu wa serikali zote kukabiliana na mauaji ya kimbari na jinai za kivita za utawala huo ghasibu.

Ismail Baqaei 

 

Aidha amekosoa vikali himaya na uungaji mkono wa kisilaha na kisiasa wa Marekani na baadhi ya mataifa ya Magharibi kwa utawala ghasibu wa Israel na kuueleza kwamba, mataifa hayo ni washirika wa uhalifu na jina za Israel.

Watu wasiopungua 93 wakiwemo wanawake na watoto wadogo waliuliwaJuumanne ya jana katika mashambulizi ya kinyama ya ndege za kivita za Israel dhidi ya jengo la ghorofa tano katika mji wa Bait Lahia kaskazini mwa Ukanda wa Gaza.

Tags