Hizbullah na Israel zavunja rekodi ya saa 24
(last modified Tue, 26 Nov 2024 02:27:02 GMT )
Nov 26, 2024 02:27 UTC
  • Hizbullah na Israel zavunja rekodi ya saa 24

Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon imevunja rekodi kwa kufanya zaidi ya operesheni 50 za kuutwanga utawala wa Kizayuni katika kipindi cha saa 24 huku Israel nayo ikivunja rekodi kwa kupiga ving'ora vingi zaidi vya hatari, suala ambalo halijawahi kutokea katika historia nzima ya utawala pandikizi wa Kizayuni.

Shirika la habari la Tasnim limeripoti kuwa, takwimu ya vipigo vilivyotolewa Jumapili na Hizbullah dhidi ya utawala wa Kizayuni zinaonesha kuwa harakati hiyo ya Muqawama wa Kiislamu hadi kufikia mwishoni mwa siku ya Jumapili ilikuwa imevunja rekodi ya operesheni zake dhidi ya utawala wa Kizayuni katika kipindi cha siku moja huku Israel nayo ikivunja rekodi za historia yake yote za kupiga ving'ora vya hatari vingi zaidi na muda mrefu zaidi siku hiyo.

Siku hiyo ya Jumapili, Hizbullah ilifanya operesheni 51 za kutoa vipigo dhidi ya Israel huku utawala wa Kizayuni nao ukipiga ving'ora kwa zaidi ya mara 500 katika kipindi cha saa 24 ikiwa ni mara ya kwanza katika historia yake na ni ushahidi wa hali mbaya sana wanayopitia walowezi wa Kizayuni katika ardhi za Palestina zilizopachikwa jina bandia la Israel.

Katika kipindi cha siku hiyo moja, Hizbullah imeteketeza magairi 6 ya deraya ya Israel, imepigwa maeneo 14 ya kijeshi ya Israel, vitongoji 14 vya waloweizi wa Kizayni na miji na maeneo 18 na mikusanyiko wanajeshi makatili wa Israel ni sehemu ya vipigo vilivyotolewa na Hizbullah dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel.

Katika kipindi cha siku tatu zilizopita, Hizbullah ya Lebanon imekuwa ikiongeza vipigo vyake dhidi ya Israel siku baada ya siku.