Hemmati: Iran imeimarika katika mfumo mpya wa dunia
(last modified Tue, 26 Nov 2024 13:31:16 GMT )
Nov 26, 2024 13:31 UTC
  • Hemmati: Iran imeimarika katika mfumo mpya wa dunia

Waziri wa Masuala ya Kiuchumi na Fedha wa Iran amesema kuongezeka kwa uwezo wa Jamhuri ya Kiislamu katika mfumo mpya wa dunia kumeiwezesha nchi hii kuchukua nafasi kubwa katika nyanja kama vile kupambana na mabadiliko ya tabianchi, uhamishaji teknolojia na uwekezaji wa pamoja.

Abdolnaser Hemmati aliyasema hayo wakati wa hotuba yake katika Mkutano wa 28 wa Uwekezaji Duniani wa Jumuiya ya Taasisi za  Kukuza Uwekezaji Duniani (WAIPA) katika mji mkuu wa Saudia, Riyadh siku ya Jumatatu.

Amesisitiza kuwa: Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa kuunda serikali ya umoja wa kitaifa ndani ya nchi na kuimarisha nafasi yake katika majukwaa ya kimataifa kama vile kujiunga rasmi na Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai (SCO) na BRICS, na vile vile kuimarisha ukuruba na ushirikiano na Umoja wa Kiuchumi wa Eurasia na nchi jirani katika Ghuba ya Uajemi, inafuatilia sera ya kuweka msingi wa ushirikiano wa pamoja."

Hemmati amesisitiza kuwa: "Uchumi wa Iran ambao una raslimali nyingi za asili, madini na nishati, vijana na watu wenye elimu, nafasi ya kipekee ya kijiografia na mtandao mpana wa miundombinu ya kiuchumi, una uwezo mkubwa wa kukabiliana na changamoto zilizopoto na kutumia fursa zinazojitokeza."

Mkutano wa nchi za BRICS

Akizungumzia suala la vikwazo vya Magharibi dhidi ya Iran, Hemmati ameonya kwamba "vikwazo vya kiuchumi sio tu vina madhara kwa Iran" bali pia athari zake za kisiasa na kiuchumi zimeenea katika "uchumi mzima wa kikanda na kimataifa."

Mkutano huo wa Riyadh ulianza Novemba 25 na unatazamiwa kumalizika kesho ambapo madaa kuu ya mkutano huo wa WAIPA, ni " Taasisi za  Kukuza Uwekezaji Duniani zilizo Tayari kwa Mustakbali: Kupitia Mfumo wa Kidijitali na Ustawi Endelevu". Mkutano huo umeandaliwa na Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji ya Saudia.