Afrika Kusini yasisitiza kuhusu kuchukuliwa hatua za kimataifa kupigania uhuru wa Palestina
(last modified Tue, 26 Nov 2024 13:26:07 GMT )
Nov 26, 2024 13:26 UTC
  • Afrika Kusini yasisitiza kuhusu kuchukuliwa hatua za kimataifa kupigania uhuru wa Palestina

Afrika Kusini Jumatatu ilisisitiza wito wake wa kusitishwa mapigano mara moja huko Palestina na Lebanon na kuanzishwa kwa mchakato wa kisiasa ili kupatikana amani ya kiadilifu na ya kudumu.

Taarifa iliyotolewa kwa ajili ya kuadhimisha Siku ya 47 ya Umoja wa Mataifa ya Kimataifa ya Mshikamano na Wananchi wa Palestina imesema kuwa: "Hafla hii (Siku ya Kimataifa ya Mshikamano na Palestina) inatupa fursa muhimu ya kutafakari na kutathmini hali mbaya ya wananchi wa Palestina."

Afrika Kusini imesisitiza dhamira yake isiyoyumba ya kuimarisha dhamana yake ya mshikamano, urafiki na ushirikiano na Palestina.

Taarifa hiyo iliongeza kuwa: "Kwa kuzingatia uungaji mkono wa muda mrefu wa Afrika Kusini kwa watu wa Palestina, Serikali ya Afrika Kusini inasalia na nia ya kuunga mkono mipango inayolenga kuelekeza tena ajenda ya kimataifa kuhusu Palestina na mchakato wa amani uliofufuliwa wa Mashariki ya Kati."

Serikali pia imeitaka jamii ya kimataifa kuzidisha juhudi za kuwasaidia Wapalestina katika kufikia matarajio yao ya uhuru, haki na uanzishwaji wa nchi huru . ya Palestina