-
Rais wa Iran awasili Pakistan katika ziara ya kuimarisha uhusiano wa kibiashara na usalama
Apr 22, 2024 06:42Rais Ebrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amewasili katika mji mkuu wa Pakistan Islamabad katika ziara rasmi ya kikazi yenye lengo la kuimarisha usalama na uhusiano wa kibiashara kati ya nchi mbili.
-
Mvua kali za mafuriko zaua watu wasiopungua 168 Pakistan na Afghanistan
Apr 20, 2024 10:41Watu wasiopungua 168 wamepoteza maisha katika matukio yaliyosababishwa na mvua, baada ya mvua kali na mafuriko kuikumba Pakistan na nchi jirani ya Afghanistan.
-
Uamuzi wa Pakistan dhidi ya harakati ya Zainabiyyun; malengo na matokeo yake
Apr 14, 2024 13:11Serikali ya Pakistan imechukua uamuzi wa kushtukiza na uliowashangaza na kuwapiga butwaa watu wengi, nao ni wa kuiweka harakati ya Zainabiyyun kwenye orodha yake ya tasisi za kigaidi licha ya kwamba harakati hiyo muda wote imekuwa ikipigania amani na usalama kwa Pakistan.
-
Watu wenye silaha waua abiria 11 kusini magharibi mwa Pakistan
Apr 14, 2024 02:30Watu wenye silaha wameua abiria wasiopungua 11 katika matukio mawili tofauti yaliyojiri kusini magharibi mwa Pakistan.
-
Raisi: Madola ya kibeberu yanazusha fitna ili kuvuruga usalama kati ya Iran na Pakistan
Apr 12, 2024 11:18Rais Ebrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema, kustawishwa uhusiano wa Iran na Pakistan hakufurahishi madola ya kibeberu na kwa hivyo yanazusha fitna ili kuleta mpasuko kati ya mataifa hayo mawili na nchi hizo mbili za Kiislamu.
-
SEPAH: Magaidi 15 wameshaangamizwa hadi hivi sasa kusini mashariki mwa Iran
Apr 04, 2024 11:38Kamanda wa Kikosi cha Nchi Kavu cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (SEPAH) amesema kuwa, hadi hivi sasa magaidi 15 wameshaangamizwa katika operesheni za kuzima mashambulizi matatu ya kigaidi yaliyofanywa na magaidi hao kusini mashariki mwa Iran.
-
Sisitizo la Pakistna la kuhitajia mno gesi ya Iran
Mar 30, 2024 02:31Musadik Masood Malik, Waziri wa Mafuta wa Pakistan amesema kuwa nchi yake inahitajia mno gesi ya Iran na kwamba msimamo wa Islamabad uko wazi kuwa, kukamilishwa mradi wa kupelekwa gesi ya Iran nchini Pakistan ni jambo la dharura.
-
Kiongozi wa kundi la kigaidi la Jaish al Dhulm aangamizwa katika hujuma ya askari usalama wa Iran
Feb 26, 2024 02:31Kiongozi wa kundi la kigaidi la "Jaish al-Dhulm" ameuawa katika shambulio la askari usalama wa Iran.
-
Matokeo ya mwisho ya uchaguzi wa Pakistan
Feb 13, 2024 07:18Tume ya Uchaguzi ya Pakistani imetangaza matokeo ya mwisho ya uchaguzi wa bunge nchini humo, na wagombea huru wenye mfungamano na chama cha Tehreek-e-Insaf cha Imran Khan wamenyakua viti 101.
-
Mamilioni ya Wapakistan wapiga kura kuchagua serikali mpya, matukio kadhaa ya mauaji yaripotiwa
Feb 08, 2024 11:33Wapakistani wapatao milioni 128 waliotimiza masharti leo wameelekea kwenye vituo vya kupigia kura katika uchaguzi mkuu muhimu wa kuchagua serikali mpya itakayoongoza nchi hiyo kwa miaka mitano ijayo, huku usalama ukiimarishwa kwa kuchukuliwa hatua kadhaa ikiwemo kusitishwa huduma za simu za mkononi na mtandao wa intaneti licha ya kuripotiwa matukio kadhaa ya mauaji.