-
Hotuba ya Amir wa Qatar katika Baraza Kuu la UN; ukosoaji wa wazi wa mapatano na Israel
Sep 25, 2020 22:59Amir wa Qatar, Sheikh Tamim bin Hamad Aal Thani amelaani hatua za Israel dhidi ya Palestina na akaeleza kwamba jamii ya kimataifa imeshindwa kukabiliana na "ukichwangumu" wa Israel.
-
Qatar nayo yakataa kuchukua uwenyekiti wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu
Sep 25, 2020 07:47Serikali ya Qatar imekataa kuchukua uwenyekiti wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu, Arab League badala ya Palestina ambayo nayo ilikataa uwenyekiti huo ikilalamikia hatua ya baadhi ya mataifa ya jumuiya hiyo ya kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Israel.
-
Hamas: Muamala wa Karne umekuwa chachu ya kuimarika harakati za mapambano za Palestina
Sep 25, 2020 03:25Mjumbe wa Idara ya Siasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) amesema kuwa njama ya Muamala wa Karne na uhasama unaofanywa dhidi ya Palestina vimekuwa chachu ya kukurubiana zaidi harakati na makundi ya kupigania ukombozi ya Palestina.
-
Amir wa Qatar na Mfalme wa Jordan wataka kuundwa taifa huru la Palestina
Sep 23, 2020 03:43Amir wa Qatar na Mfalme wa Jordan wamesisitiza udharura wa kuundwa taifa huru la Palestina, huku wakikosoa kimya cha jamii ya kimataifa mkabala wa ukaliaji mabavu wa ardhi za Wapalestina.
-
Palestina yakataa kuchukua uwenyekiti wa Arab League
Sep 22, 2020 08:05Waziri wa Mambo ya Nje wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina amesema kuwa mamlaka hiyo imeamua kusamehe haki yake ya kuwa mwenyekiti wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu, Arab League.
-
Yaliyomo kwenye mpango wa Marekani wa kutaka kumuengua Mahmoud Abbas
Sep 20, 2020 03:31David Friedman, Balozi wa Marekani katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu (Israel) Alhamisi iliyopita alisema kuwa; Marekani inafikiria kumweka Mohammed Dahlan, kiongozi wa zamani wa harakati ya Fat-h kwenye uongozi wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina kuchukua nafasi ya Mahmoud Abbas, rais wa sasa wa mamlaka hiyo.
-
Wall Street Journal: Mfalme Salman ametofautiana na mrithi wake kuhusu kuanzisha uhusiano na Israel
Sep 19, 2020 22:08Gazeti la Wall Street Journal la Marekani limefichua kuwa, kumetokea hitilafu kubwa na kali baina ya Mfalme Salman bin Abdulaziz Al Saud wa Saudi Arabia na mrithi wake, Muhammad bin Salman baada ya mapatano ya Imarati na utawala wa Kizayuni wa Israel ya kuanzisha uhusiano wa kidiplomasia baina ya pande hizo mbili.
-
Iran: Njia yoyote ya uchukuaji hatua inayopuuza matakwa ya taifa la Palestina ni batili
Sep 19, 2020 00:03Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imetangaza kuwa: Njia yoyote ile ya uchukuaji hatua ikiwemo ya "Muamala wa Karne" ambayo haitatilia maanani matakwa ya taifa la Palestina ni batili.
-
Tofauti baina ya Mapatano ya Abraham, Camp David na Wadi Araba
Sep 18, 2020 03:40Nchi za Kiarabu zimesaini mapatano mara tatu na utawala wa Kizayuni wa Israel na ya hivi karibuni zaidi kati ya mapatano hayo ni yale yliyopewa jina la Mapatano ya Abraham (Abraham Accords) yaliyosainiwa tarehe 15 mwezi huu wa Septemba katika Ikulu ya Rais wa Marekani, White House. Mapatano hayo matatu yana tofauti kadhaa na muhimu.
-
Russia: Amani haitapatikana Asia Magharibi bila kutatuliwa kadhia ya Palestina
Sep 18, 2020 03:36Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia imesema ni kosa kudhani kuwa amani ya kudumu itapatikana katika eneo la Asia Magharibi pasi na kutatuliwa mgogoro wa Palestina.