-
Netanyahu aapa hakutakuwa na Dola la Palestina, asisitiza ardhi yote ni milki ya wazayuni
Sep 12, 2025 10:28Waziri mkuu wa utawala wa kizayuni wa Israel Benjamin Netanyahu ameapa kuwa, hakutakuwa na dola la Palestina, na kusisitiza kwamba ardhi zote za Wapalestina zinazokaliwa kwa mabavu na utawala huo haramu ni milki ya wazayuni.
-
Bunge la Ulaya lataka kutambuliwa rasmi Palestina Huru
Sep 12, 2025 06:37Bunge la Ulaya limepasisha azimio likielezea wasiwasi wake kuhusu hali mbaya ya Ukanda wa Gaza, na kuzitaka nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya kuliweka suala la kutambuliwa taifa huru la Palestina kwenye ajenda.
-
Uhispania yamuita nyumbani balozi wake wa Israel
Sep 10, 2025 06:40Vyombo vya habari vya Uingereza vimeripoti kuwa Uhispania imemuita tena balozi wake katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu (Israel) ikilalamikia sera za mauaji za Israel katika Ukanda wa Gaza.
-
Netanyahu na jeshi la kizayuni watoa vitisho vikali kwa Wapalestina: Ondokeni Ghaza sasa hivi!
Sep 09, 2025 10:28Waziri mkuu wa utawala wa kizayuni wa Israel Benjamin Netanyahu ametishia kile anachokiita operesheni kali ya ardhini katika mji wa Ghaza, huku akitoa vitisho kwa Wapalestina walioko katika mji huo kwa kuwataka waondoke sasa hivi.
-
Uhispania yataka Israel ifukuzwe kwenye mashindano ya baiskeli
Sep 06, 2025 11:29Waziri wa Mambo ya Nje wa Uhispania ameunga mkono wito wa kuondolewa timu ya waendesha baiskeli ya Israel kwenye mashindano ya mchezo huo yanayoendelea, kufuatia maandamano na malalamiko ya waungaji mkono wa Palestina nchini humo.
-
Mkurugenzi wa klabu ya michezo ya Gaza auawa katika shambulilo la Israel akisubiri misaada
Sep 02, 2025 11:20Shambulizi la anga la Israel ambalo lililenga umati wa watu waliokuwa wakisubiri misaada ya kibinadamu kaskazini mwa Gaza limemuua pia Louay Estita, Mkurugenzi wa Klabu ya Michezo ya Gaza.
-
Msimamo wa karibuni wa Malaysia kuhusiana na utawala wa kizayuni na jinai unazofanya Ghaza
Sep 01, 2025 07:24Malaysia imeitaka Jamii ya Kimataifa isimamishe uwanachama wa utawala wa Kizayuni wa Israel katika Umoja wa Mataifa na kuuwekea vikwazo vikali utawala huo ghasibu.
-
US yawazuia viongozi wa PLO na PA kuhudhuria UNGA huku nchi zikijiandaa kuitambua Palestina
Aug 30, 2025 05:53Marekani imebatilisha rasmi viza za maafisa wa Palestina, na kuwazuia kuhudhuria Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UNGA) utakaofanyika mwezi ujao wa Septemba mjini New York, makao makuu ya umoja huo, hatua ambayo inakuja wakati nchi kadhaa za Magharibi zinajiandaa kuitambua nchi ya Palestina.
-
Waislamu Nigeria wataka kuachiwa huru kiongozi wa Palestina
Aug 29, 2025 02:24Harakati ya Kiislamu ya Nigeria imelaani vikali hatua ya polisi ya Nigeria kumkata kiongozi wa Jumuiya ya Wapalestina katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi, Ramzy Abu Ibrahim, ikisisitiza kuwa kukamatwa huko kunafungamana na makubaliano ya hivi karibuni ya usalama kati ya Nigeria na utawala wa Israel.
-
WHO: Zaidi ya watu 15,600 wakiwemo watoto 3,800 wanahitaji kuondolewa haraka Gaza kwa ajili ya matibabu
Aug 24, 2025 11:53Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) ameeleza kuwa watu zaidi ya 15,600 katika Ukanda wa Gaza, wakiwemo watoto 3,800, wanahitaji kuondolewa haraka katika eneo hilo lililokumbwa na vita ili kupata huduma maalumu ya matibabu.