Taasisi za Palestina: Maelfu ya wafungwa wanateswa katika magereza ya Israel
https://parstoday.ir/sw/news/daily_news-i134778-taasisi_za_palestina_maelfu_ya_wafungwa_wanateswa_katika_magereza_ya_israel
Asasi mbili za Kipalestina yametangaza kwamba, zaidi ya mateka na wafungwa 9,300 wa Palestina wanaoshikiliwa katika magereza na vituo vya kuzuiliwa vya Israel wanakabiliwa na "mateso yaliyopangwa."
(last modified 2026-01-03T13:29:21+00:00 )
Dec 27, 2025 06:01 UTC
  • Taasisi za Palestina: Maelfu ya wafungwa wanateswa katika magereza ya Israel
    Taasisi za Palestina: Maelfu ya wafungwa wanateswa katika magereza ya Israel

Asasi mbili za Kipalestina yametangaza kwamba, zaidi ya mateka na wafungwa 9,300 wa Palestina wanaoshikiliwa katika magereza na vituo vya kuzuiliwa vya Israel wanakabiliwa na "mateso yaliyopangwa."

Shirika la Masuala ya Mateka na Waachiliwa Huru wa Kipalestina lenye mfungamano na Harakati ya ukombozi wa Palestina pamoja na Klabu ya Wafungwa wa Palestina yametangaza katika taarifa kwamba, Wapalestina hao wanakabiliwa na "ongezeko linaloendelea la hatua za ukandamizaji" katika magereza ya Kizayuni, ikiwa ni pamoja na kupigwa, matumizi ya mabomu ya kushtua, mbwa wa polisi, mshtuko wa umeme, na kunyimwa haki ya wafungwa kupata hewa safi na mahitaji ya msingi, ikiwa ni pamoja na chakula, huduma ya matibabu, na mavazi.