Vita vya kieneo; maana yake na jinsi vinavyotokea?
Kwa mujibu wa ripoti ya Pars Today, kutokana na uchochezi na vitisho vya mara kwa mara vya Marekani dhidi ya Iran, Tehran imeonya kwamba shambulio lolote la kijeshi kutoka Marekani dhidi ya Iran litasababisha kuwashwa moto wa vita vya eneo. Sasa swali linaibuka: vita vya eneo ni nini na vinafanyika vipi?
Vita vya eneo ni aina ya mapambano ya kijeshi ambayo havibaki kati ya nchi mbili tu zinazohasimiana, bali huenea kijiografia na kuhusisha maeneo mengi katika eneo zima. Huingiza nchi na wahusika wengi, ima moja kwa moja au kwa njia isiyo ya moja kwa moja na matokeo yake hutoka nje ya mipaka ya uwanja mkuu wa vita.
Kwa kawaida, vita vya aina hii huanza kutoka pande kadhaa kwa wakati mmoja, na mwisho wake huwa haviwezi kudhibitiwa na wahusika wanaopigana. Ili kufahamu vyema asili na mwenendo wa tukio hili, vinaweza kuchambuliwa kwa vipengele vinne vikuu.
Kuenea kwa kijiografia na kuwa na ngazi nyingi za vita:
Sifa ya kwanza ya vita vya kikanda ni pale inapozidi mipaka ya nchi mbili zinazohasimian. Mgogoro hupanuka haraka hadi nchi nyingine au serikali za kikanda. Kwa mfano, mzozo wa awali kati ya nchi mbili unaweza kuibuka kwa sababu ya kuwepo kwa kambi za kijeshi za upande mmoja katika nchi ya tatu, au kutokana na ahadi za usalama, au uwepo wa nguvu za kimataifa zinazohusiana na eneo hilo. Katika hali hii, siyo kambi za kijeshi tu, bali kila nchi au utawala husika hutoa ardhi, anga au rasilimali zake kwa upande mmoja huhesabiwa kama sehemu ya uwanja wa vita. Hali hii inasababisha kuundika kwa ngazi nyingi za mapambano katika maeneo tofauti kijiografia na kuondoa uwezekano wa kusimamia au kupunguza eneo la mgongano.
Uwepo na wahusika wengi:
Wahusika katika vita vya kikanda hawako tu katika jeshi rasmi la serikali. Mitandao ya kikanda, makundi ya Muqawama au wapigania ukombozi, nguvu za kigeni zinazotumika kwa njia ya niaba, na miungano ya kimataifa huweza kuingia kikamilifu katika mzozo. Hii inafanya vita kuondoka kwenye mfumo wa mapambano ya kawaida yenye usawa, na kuyabadilisha kuwa mgogoro changamano, usio sawa na mkubwa zaidi. Katika hali hii, nchi moja inaweza isiwe moja kwa moja katika mapambano ya uso kwa uso, lakini mtandao wa washirika wake au makundi yanayoiunga mkono katika kanda yote yanaweza kuingilia kati, na kimsingi kuifanya nchi hiyo kushiriki katika vita vya pande nyingi.
Mzozo usio sawa (usio simetria):
Vita vya kikanda si lazima viwe vya mlingano wa usawa. Inawezekana upande mmoja utategemea faida ya kiteknolojia, angani na baharini kujaribu kumaliza vita haraka au kwa muda mfupi, wakati upande mwingine ukitumia kina cha kimkakati, eneo kubwa kijiografia, uwezo wa makombora na ndege zisizo na rubani, pamoja na silaha kama vile vita vya mtandao (cyber) na kutatiza njia muhimu za usafirishaji (kama vile barabara za kimataifa). Hii hii hupelekea kukosekana mlingano katika vita. Katika hali hii, vita vinaweza kufafanuliwa kama “vita ya kijiografia dhidi ya teknolojia” au kuingilia kati miundombinu muhimu ya uchumi na nishati, na kufanya upande wenye teknolojia ya hali ya juu kuwa hatarini.
Madhara ya mipaka ya kimataifa na kwa wananchi:
Sifa muhimu zaidi ya vita vya kikanda ni upanuzi wa madhara yake. Athari za vita kama hivi si za kijeshi pekee; vipengele vya usalama, uchumi na siasa vinapita mipaka kwa haraka.
Kutokuwa na usalama katika njia muhimu za usafirishaji wa nishati na biashara ya kimataifa kunaweza kusababisha usumbufu wa ugavi wa rasilimali na kuongezeka kwa bei kwa kiwango kikubwa, na kuweka shinikizo juu ya uchumi wa dunia. Kwa mfano, kutokuwa na usalama katika njia muhimu kama Lango Bahari la Hormuz, ambapo takriban asilimia 20 ya nishati ya dunia hupita, kunakuwa na athari ya moja kwa moja na haraka kwa uchumi wa nchi zote zinazotegemea mafuta. Zaidi ya hayo, vita hivi vinaweza kuamsha migawanyiko ya kikabila, kidini na ya kifikra iliyoingia ndani ya kanda, na kuendeleza kutokuwa na utulivu kwa miongo kadhaa.
Onyo kuhusu vita vya kikanda:
Inaonekana kuwa vita vya kikanda si tu vita vikubwa zaidi, bali ni mabadiliko ya kimsingi katika asili ya mzozo. Hii ni kwa sababu kuna uwezekano mkubwa kwamba wigo wa vita hivi hauwezi kudhibitiwa na pande husika na wahusika wasio wa serikali na wa kikanda watakuwa na nafasi muhimu. Aidha mbinu za mapambano zisizo sawa na zisizo za kawaida zitazidi kutumika, na madhara yake yataathiri nchi zote za kanda na hata jamii ya kimataifa kwa kiasi kikubwa. Sifa hizi za vita vya kikanda zinaonyesha kwa nini onyo kuhusu mzozo kugeuka kuwa vita vya kikanda ni onyo la kimkakati kuhusu kutoweza kudhibiti matokeo yake.
Kwa kuzingatia ongezeko la vitisho vya kijeshi vya Washington dhidi ya Tehran na kuongezwa kwa wanajeshi na vifaa vya kijeshi vya Marekani na waitifaki wake katika eneo la Asia Magharibi, maafisa wa ngazi ya juu wa Iran wametoa onyo kuhusu uwezekano wa mashambulizi yoyote ya Marekani dhidi ya Iran kugeuka kuwa vita vya kikanda.
Katika muktadha huu, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Khamenei, mnamo Februari 1, 2026, alisema katika hotuba yake kwamba jitihada za Marekani za “kuimeza” Iran na msimamo thabiti wa taifa la Iran dhidi ya tamaa hiyo ndio chanzo kikuu cha mzozo wa miaka 47 kati ya Iran na Marekani.
Akirejelea maneno ya hivi karibuni ya Marekani, aliongeza: “Katika kuwafanya Wairani waogope, wamekuwa wakisema ‘chaguzi zote ziko mezani,’ lakini wajue kwamba iwapo wataanzisha vita sasa, basi vitakuwa ‘vita vya kikanda.’”