-
Wacanada waandamana wakimtaka Trudeau aache kuiuzia Israel silaha
Dec 13, 2023 07:45Waungaji mkono wa Palestina wanaoishi nchini Canada wamefanya maandamano makubwa kulaani jinai za Wazayuni dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza, ambapo mbali na kuonyesha mshikamano wao na wakazi wa Gaza, lakini pia wamemtaka Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Justin Trudeau kuacha kuuuzia silaha utawala wa Kizayuni.
-
Abdollahian: Unyama wa utawala wa Israel huko Gaza una utambulisho wa Kidaesh
Dec 13, 2023 01:01Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran amesema: Mienendo isiyo ya kibinadamu ya utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya raia mateka wa Palestina katika ukanda wa Gaza ni mfano na ishara ya wazi ya tabia ya kundi la kigaidi la Daesh.
-
Jeshi la Yemen: Tumeshambulia kwa kombora meli iliyokuwa ikielekea Israel
Dec 12, 2023 23:16Vikosi vya ulinzi vya Yemen vimekiri kuhusika na shambulizi la kombora la cruise dhidi ya meli ya mafuta katika Bahari Nyekundu, ikiwa njiani kuelekea katika bandari ya utawala wa Kizayuni wa Israel.
-
Uchunguzi wa maoni: Wamarekani wengi wanapinga sera ya Biden kuhusu vita vya Gaza
Dec 11, 2023 23:29Uchunguzi wa maoni uliofanywa na televisheni ya Marekani ya CBS News umeonyesha kuwa asilimia kubwa ya Wamarekani wanapinga jinsi Rais Joe Biden anavyoshughulikia vita vya Israel dhidi ya watu wa Ukanda wa Gaza.
-
Raisi: Kimbunga cha al-Aqsa kimepanua mipaka ya muqawama
Dec 10, 2023 00:31Rais wa Iran amesema Operesheni ya Kimbunga cha al-Aqsa imepanua mipaka ya muqawama na kuufikisha katika kona zote za dunia.
-
Makundi ya muqawama yatoa mwito wa kufanyika 'mgomo wa ulimwengu'
Dec 10, 2023 00:31Muungano wa makundi ya muqawama wa Palestina umetoa mwito wa kufanyika 'mgomo kamili wa kimataifa' kwa ajili ya kuonyesha mshikamano na wananchi wa Palestina katika Ukanda wa Gaza, ambao wanakabiliwa na mauaji ya kimbari ya utawala wa Kizayuni wa Israel kwa zaidi ya miezi miwili sasa.
-
Mufti wa Oman alaani wanaotaka kudhoofisha muqawama wa Wapalestina
Dec 09, 2023 23:37Mufti Mkuu wa Oman amewakosoa wale wanaojaribu kudhoofisha harakati za mapambano ya Kiislamu (muqawama) za Wapalestina dhidi ya jinai za utawala haramu wa Israel.
-
Ripoti: Israel imeua makumi ya wanariadha wa Palestina tangu Oktoba 7
Dec 09, 2023 23:25Israel imeua shahidi makumi ya wanariadha na wamamichezo wa Palestina tangu utawala huo wa Kizayuni uanzishe mashambulizi ya kutisha dhidi ya Ukanda wa Gaza mnamo Oktoba 7.
-
HAMAS yaendelea kujibu jinai za Wazayuni, Israel yakiri kujeruhiwa maelfu ya wanajeshi wake
Dec 09, 2023 11:33Wanamapambano wa Brigedi za Izzuddin al Qassam, Tawi la Kijeshi la Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS wametangaza leo kuwa wameendelea kuvipiga kwa makombora vitongoji vya walowezi wa Kizayuni kikiwemo kitongoji cha Magin (ماگین).
-
HAMAS yalaani kitendo cha askari wa Israel cha kuwakashifu Wapalestina kwa kuwavua nguo hadharani
Dec 09, 2023 02:49Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS imelaani kitendo cha wanajeshi wa utawala haramu wa Kizayuni wa Israel cha kuwalazimisha kuvua nguo Wapalestina wapatao 100 waliowakamata; na kuwakashifu kwa kuwaweka hadharani katika barabara za Ukanda wa Gaza wakiwa wamebaki na nguo za ndani tu.