-
UN yataka kuchunguzwa ukatili wa Wazayuni katika Msikiti wa Al-Aqsa
Apr 23, 2022 08:58Msemaji wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA) ametoa wito wa kufanyika uchunguzi wa haraka na wa wazi kuhusiana na mashambulio ya kikatili ya wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya waumini wa Kipalestina waliokuwa wakifanya ibada katika Msikiti wa Al-Aqsa.
-
Sisitizo la Iran la kurudishwa amani ya kudumu katika eneo kwa kuondolewa ukaliwaji mabavu wa ardhi za Palestina
Apr 22, 2022 03:46Hussein Amir Abdollahian, Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa amani ya kudumu katika eneo la Asia Magharibi itapatikana tu kwa kuondolewa kikamilifu ukaliwaji mabavu wa ardhi za Palestina, kurejea wakimbizi wote katika ardhi zao za jadi na kuainishwa mfumo wa utawala wa baadaye wa Palestina kwa msingi wa kura ya maoni pamoja na kuundwa serikali huru katika ardhi hizo.
-
Faisal Miqdad: Marekani na nchi za Magharibi zinafanya njama za kuangamiza suala la Palestina
Apr 22, 2022 02:40Waziri wa Mambo ya Nje wa Syria amesema kuwa, nchi za Magharibi zinaendelea kula njama za kuvuruga na kuharibu kadhia ya ukombozi wa Palestina na haki thabiti za watu wake, hususan haki ya wakimbizi wa Kipalestina kurejea katika nchi yao na kuongeza kuwa, Damascus inafuatilia kwa wasiwas matukio hatari yanayojiri huko Quds ( Jerusalem) inayokaliwa kwa mabavu.
-
Mufti wa Oman awakosoa viongozi wa Kiarabu wanaofuturu na Wazayuni huku al Aqsa ikitiwa najisi
Apr 20, 2022 22:19Mufti Mkuu wa Oman, Sheikh Ahmed bin Hamad al-Khalili, amepongeza misimamo ya kishujaa ya wanamapambano wanaoendelea kukabiliana na uvamizi wa mara kwa mara wa Israel katika Msikiti wa Al-Aqsa katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani.
-
Wataliano waandamana kulaani mashambulizi dhidi ya Wapalestina al-Aqsa
Apr 19, 2022 02:55Maandamano makubwa yamefanyika katika mji mkuu wa Italia, Rome ya kulaani mashambulio ya wanajeshi makatili wa Israel dhidi ya Wapalestina katika Msikiti wa al-Aqsa ulioko katika mji mtukufu wa Quds unaokaliwa kwa mabavu.
-
HAMAS: Muqawama ndiyo njia ya kimsingi zaidi ya kuihami Quds Tukufu
Apr 18, 2022 22:30Mmoja wa viongozi wa ngazi za juu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS amesema kuwa, Baytul Muqaddas ndio mji mkuu wa milele wa Palestina na kusisitiza kuwa, kinachoifanya Quds ibakie ni kuendelezwa muqawama mbele ya adui vamizi.
-
Sudan yaitaka jamii ya kimataifa kuiwajibisha Israel baada ya kuvamia al Aqsa
Apr 18, 2022 08:38Wizara ya Mambo ya Nje ya Sudan imelaani vikali mashambulizi ya wanajeshi wa Israel dhidi ya Msikiti wa Al-Aqsa na shambulio dhidi ya waumini wa Kipalestina wasio na ulinzi waliokuwa wakitekeleza ibada ya Swala ya Alfajiri katika eneo hilo.
-
Wamorocco, Wabahrain, Waturuki waandamana kuitetea Aqsa, Syria, Kuwait zatoa kauli
Apr 17, 2022 03:47Wananchi wa Morocco wamefanya maandamano makubwa katika mji mkuu wa nchi hiyo, Rabat kutangaza uungaji mkono wao kwa wananchi wa Palestina, sanjari na kulaani kitendo cha utawala haramu wa Israel cha kuuvamia na kuuvunjia heshima Msikiti wa al-Aqsa.
-
Iran yawaasa Waislamu duniani waungane kuwatetea Wapalestina, Msikiti wa Aqsa
Apr 16, 2022 22:56Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran kwa mara nyingine tena amelaani jinai ya utawala wa Kizayuni wa Israel ya kuushambulia na kuuvunjia heshima Msikiti wa al-Aqsa na kusisitiza kuwa, mataifa ya Kiislamu yanapaswa kuungana na kusima bega kwa bega kuitetea kadhia ya Palestina.
-
Iran: Israel ni dhaifu, haiwezi kuhimili nguvu za muqawama wa Palestina
Apr 16, 2022 05:58Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran sambamba na kulaani kitendo cha wanajeshi wa Israel kuvamia viwanja vya Msikiti wa Al-Aqsa na kuvunjia heshima kibla cha kwanza cha Waislamu, amesisitiza kuwa utawala huo wa Kizayuni ni dhaifu, na wala hauna ubavu wa kustahamili nguvu za mrengo wa muqawama wa Palestina.