Abdollahian: Iran itaendelea kuunga mkono muqawama wa Palestina
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i84464-abdollahian_iran_itaendelea_kuunga_mkono_muqawama_wa_palestina
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema Jamhuri ya Kiislamu katu haitoruhusu kukanyagwa haki za Wairani katika mazungumzo (ya Vienna) au kupuuza haki za wananchi Waislamu wa Palestina na kueleza bayana kuwa, Tehran itaendelea kuunga mkono muqawama wa Wapalestina.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 06, 2022 23:03 UTC
  • Abdollahian: Iran itaendelea kuunga mkono muqawama wa Palestina

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema Jamhuri ya Kiislamu katu haitoruhusu kukanyagwa haki za Wairani katika mazungumzo (ya Vienna) au kupuuza haki za wananchi Waislamu wa Palestina na kueleza bayana kuwa, Tehran itaendelea kuunga mkono muqawama wa Wapalestina.

Hossein Amir-Abdollahian alisema hayo jana Jumatatu katika mazungumzo yake na viongozi wa kisiasa na maafisa kutoka makundi ya muqawama ya Palestina na Lebanon, ambao wapo nchini Iran kuhudhuria kumbukumbu ya miaka 33 ya kuaga dunia Imam Ruhullah Khomeini (MA) muasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Abdollahian ameashiria mtazamo mpana wa Imam Khomeini kuhusiana na kadhia ya Palestina na kueleza kuwa, Imam Ruhullah alikuwa inaitakidi kuwa, Palestina ndiyo kadhia kuu zaidi katika ulimwengu wa Kiislamu.

Mwanadiplomasia huyo wa ngazi ya juu wa Iran amebainisha kuwa, sanjari na kuwa na mtazamo mmoja na muasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Ayatullah Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran pia amekuwa akisisitizia udharura wa kukombolewa Wapalestina akiamini kwamba, ardhi zote za Palestina zitakombolewa kutoka kwa Wazayuni maghasibu.

Amir-Abdollahian na viongozi wa kisiasa na maafisa kutoka makundi ya muqawama ya Palestina na Lebanon,

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesisitiza kuwa, katu Jamhuri ya Kiislamu haitotetereka au kuachana na msimamo wake wa kuliunga mkono na kulitetea taifa la Palestina licha ya mashinikizo ya kila upande.

Kadhalika ametaja hatua ya baadhi ya nchi za Kiislamu ya kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Israel kama usaliti na kubainisha kuwa, madola hayo yatajuta kwa maamuzi yao hayo.