-
Rouhani: Nia ya Iran ni kuwa na uhusiano wa kiudugu na nchi za pembezoni mwa Ghuba ya Uajemi
Nov 26, 2020 00:24Rais Hassan Rouhani amesema uhusiano wa Iran na Qatar ni wa kirafiki na unaendelea kustawi na akasisitiza kwamba inachotaka Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni kuwa na mazungumzo, maelewano na uhusiano wa kiudugu na nchi za pembezoni mwa Ghuba ya Uajemi.
-
Amir wa Qatar asisitiza kuimarishwa uhusiano na Iran
Nov 10, 2020 01:11Amir wa Qatar Sheikh Tamim bin Hamad al-Thani ametaka kuimarishwa uhusiano wa nchi yake na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
-
Hotuba ya Amir wa Qatar katika Baraza Kuu la UN; ukosoaji wa wazi wa mapatano na Israel
Sep 25, 2020 22:59Amir wa Qatar, Sheikh Tamim bin Hamad Aal Thani amelaani hatua za Israel dhidi ya Palestina na akaeleza kwamba jamii ya kimataifa imeshindwa kukabiliana na "ukichwangumu" wa Israel.
-
Qatar nayo yakataa kuchukua uwenyekiti wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu
Sep 25, 2020 07:47Serikali ya Qatar imekataa kuchukua uwenyekiti wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu, Arab League badala ya Palestina ambayo nayo ilikataa uwenyekiti huo ikilalamikia hatua ya baadhi ya mataifa ya jumuiya hiyo ya kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Israel.
-
Amir wa Qatar na Mfalme wa Jordan wataka kuundwa taifa huru la Palestina
Sep 23, 2020 03:43Amir wa Qatar na Mfalme wa Jordan wamesisitiza udharura wa kuundwa taifa huru la Palestina, huku wakikosoa kimya cha jamii ya kimataifa mkabala wa ukaliaji mabavu wa ardhi za Wapalestina.
-
Abdullah Abdullah: Mazungumzo ya amani na Taliban ni magumu
Sep 18, 2020 23:58Mkuu wa Baraza la Maslahi ya Taifa la Afghanistan amesema, mazungumzo ya amani baina ya Waafghani wanayofanya wao na kundi la Taliban ni magumu.
-
Uturuki, Qatar na Libya kushirikiana kijeshi
Aug 18, 2020 10:13Serikali ya Mwafaka wa Kitaifa ya Libya imesema imefikiana na Uturuki na Qatar juu ya kutia saini mkataba wa pande tatu wa ushirikiano wa kijeshi na kwamba miongoni mwa nukta muhimu za ushirikiano huo ni kujenga kituo cha kijeshi cha Uturuki katika Bandari ya Misrata nchini Libya.
-
Radiamali ya Qatar kwa njama ya Saudia ya kupanga kuishambulia kijeshi nchi hiyo
Aug 09, 2020 23:56Qatar imejibu taarifa iliyofichuliwa na jarida la Foreign Policy linalochapishwa nchini Marekani kuhusu pendekeo lililotolewa na Saudi Arabia kwa Marekani la kuiomba iishambulie Qatar na kutangaza kuwa kutokanusha suala hilo kunamaanisha kuwa Saudi Arabia ilikuwa kweli na nia ya kuishambulia Qatar.
-
Qatar: Kutokanusha Saudia ni ithibati kwamba ilikuwa na mpango wa kutushambulia kijeshi
Aug 09, 2020 03:43Kufuatia ripoti ya jarida la Foreign Policy iliyofichua kwamba Saudi Arabia ilikuwa na mpango wa kuishambulia kijeshi Qatar, Mkuu wa ofisi ya habari katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Qatar amesema, kutokadhibishwa habari hiyo na Saudia kunathibitisha ukweli wa suala hilo.
-
Uamuzi wa mahakama ya ICJ ni ushindi kwa Qatar na kushindwa kwingine kwa Saudia
Jul 15, 2020 22:06Mahakama ya Kimataifa ya Uadilifu ICJ, yenye makao makuu yake huko The Hague nchini Uholanzi imetoa hukumu kwa maslahi ya Qatar katika mzozo wa anga baina yake na nchi nyingine nne za Kiarabu.