-
Kiongozi wa HAMAS: Iran ni nchi muhimu na mhimili wa msingi katika eneo
Jun 11, 2018 10:30Mkuu wa ofisi ya kisiasa ya Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina (HAMAS) ameuenzi na kuusifu mchango wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika kuihami na kuiunga mkono Palestina na kusisitiza kwamba: Hamas haiungi mkono mhimili wowote wa Kiarabu au wa kieneo dhidi ya mhimili mwengine.
-
Qatar: Saudia iache kuingiza masuala ya dini katika mgogoro wa kisiasa
Jun 06, 2018 09:50Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu nchini Qatar sambamba na kuelezea mwenendo wa vizuizi vinavyofanywa na Saudia kwa ajili ya kuwazuia raia wa nchi hiyo kuweza kushiriki ibada ya hija, imeitaka Riyadh kuacha kuyaingiza masuala ya kidini katika mgogoro wa kisiasa wa pande mbili.
-
Mwaka mmoja wa mgogoro kati ya nchi za Kiarabu
Jun 06, 2018 01:27Umetimia mwaka mmoja tokea uanze mgogoro baina ya nchi za Kiarabu na dalili zote zinaonyesha kuwa mgogoro huo ungali unaendelea bali hata utazidi kupanuka na kuwa mbaya zaidi.
-
Qatar: Mliotuwekea vikwazo acheni ndoto za alinacha
Jun 05, 2018 09:33Katika hali inayoonekana ni ya kutoweka matumaini ya kutatuliwa hivi karibuni mgogoro wa Qatar na nchi nne za Kiarabu, waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo amesema katika kumbukumbu ya mwaka mmoja tangu Doha ianze kuwekewa vikwazo, kwamba nchi nne za Saudia, Imarati, Misri na Bahrain ziache ndoto za alinacha na njozi zisizoagulika.
-
Waziri wa Ulinzi wa Qatar: Hatutashiriki katika vita vyovyote dhidi ya Iran
Jun 04, 2018 01:29Khalid bin Mohammad Al Attiyah, Naibu Waziri Mkuu wa Qatar ambaye pia ni Waziri wa Ulinzi wa nchi hiyo amesema kuwa nchi yake haitoshiriki katika vita vyovyote dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kuongeza kwamba, haamini kuwa Marekani pia itatekeleza vita vya namna hiyo dhidi ya Tehran.
-
Saudia yatishia kuishambulia kijeshi Qatar iwapo itanunua S-400 kutoka Russia
Jun 02, 2018 03:27Mfalme Salman Bin Abdul Aziz Aal-Saud wa Saudi Arabia ametishia kuwa Riyadh itachukua hatua za kijeshi dhidi ya Qatar iwapo serikali ya Doha itaendelea na mpango wake wa kununua mfumo wa makombora wa S-400 kutoka Russia.
-
Mgogoro wa Qatar na nchi za Kiarabu wazidi kutokota, Doha yapiga marufuku bidhaa za Saudia, Imarati, Bahrain na Misri
May 27, 2018 00:13Katika hali inayoonekana ni kuzidi kuwa mkubwa mgogoro wa Qatar na nchi nne za Kiarabu zilizoizingira kila upande nchini hiyo, wizara ya uchumi na biashara ya Qatar jana ilipiga marufuku kuhifadhi, kunua na kuuza bidhaa yoyote iliyotengenezwa Saudi Arabia, Umoja wa Falme za Kiarabu yaani Imarati, Bahrain na Misri.
-
Mwanamfalme wa Qatar: Saudia iliyoiuza al-Aqsa kwa adui, haina haki ya kusimamia al-Kaabah
May 19, 2018 09:35Mjukuu wa mwasisi wa taifa la Qatar sambamba na kukosoa vikali mienendo ya Mfalme Salman bin Abdulaziz Al Saud wa Saudi Arabia kwa kuitumikia Marekani na utawala wa Kizayuni, amesema kuwa mtu ambaye ameiuza Masjidul-Aqsa kwa adui wa Uislamu, hafai kuwa msimamizi wa nyumba ya Mwenyezi Mungu ya al-Kaabah.
-
Qatar kuendelea kuisaidia Somalia huku mgogoro na Imarati ukitokota
May 15, 2018 09:14Qatar imeahidi kuendelea kuunga mkono jitihada za serikali ya Somalia za kurejesha uthabiti na uhuru wa kujitawala huku mgogoro kati ya nchi hiyo ya Pembe ya Afrika na Umoja wa Falme za Kiarabu ukiendelea kutokota.
-
Waziri wa Mambo ya Nje wa Qatar: mzingiro dhidi ya Qatar ni kwa ajili ya kuficha matatizo ya ndani Saudia
May 13, 2018 11:12Waziri wa Mambo ya Nje wa Qatar amesema kuwa sababu iliyopelekea nchi yake kuwekewa mzingiro ni kutaka kuficha matatizo ya matukio ya ndani ya Saudi Arabia, Imarati na Bahrain.