-
Kuunga mkono Russia ubunifu wa Iran wa kupunguza hali ya taharuki Ghuba ya Uajemi
May 28, 2019 07:00Ili kufikia malengo yake haramu katika eneo la Asia Magharibi na Ghuba ya Uajemi, Marekani daima imekuwa ikieneza chuki dhidi ya Iran yaani Iranophobia, na kwa njia hiyo imeibua hitilafu na mgogoro katika uhusiano wa Iran na majirani zake katika Ghuba ya Uajemi. Pamoja na hayo Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imekuwa ikisisitiza kuhusu ulazima wa kuwepo uthabiti katika Ghuba ya Uajemi na hata imewasilisha mpango mpya kuhusiana na hilo.
-
Mamufti Russia wawataka Waislamu duniani kuzuia mpango wa Marekani na Israel wa 'Muamala wa Karne'
May 25, 2019 21:56Mkuu wa Baraza la Mamufti nchini Russia amewataka Waislamu duniani kuzuia utekelezwaji wa mpango wa Marekani na utawala haramu wa Kizayuni wa Israel unaoitwa 'Muamala wa Karne' ambao kimsingi ni kulifanyia khiyana ya wazi taifa la Palestina.
-
Russia: Misimamo ya Moscow mkabala na Tehran haijabadilika
May 24, 2019 23:32Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia amesisitiza kuwa misimamo ya nchi hiyo mkabala na Iran haijabadilika baada ya Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Marekani kufanya ziara mjini Moscow.
-
Sisitizo la viongozi wa Russia, Ujerumani na Ufaransa la kulindwa mapatano ya JCPOA
May 22, 2019 05:18Mapatano ya nyuklia yanayojulikana kwa jina la JCPOA yalifikiwa mwezi Julai 2015 mjini Vienna Austria baina ya Iran na kundi la 5+1 lililojumuisha nchi za Marekani, Uingereza, Ufaransa, Russia, China pamoja na Ujerumani na Umoja wa Ulaya. Mapatano hayo yalianza kutekelezwa mwezi Januari 2016.
-
Russia, Ujerumani na Ufaransa zasisitiza kuwa JCPOA lazima ilindwe
May 22, 2019 03:46Viongozi wa Russia, Ujerumani na Ufaransa wamesisitizia haja ya kubakishwa hai na kulindwa makubaliano ya nyuklia ya JCPOA, huku wakibainisha kuwa nchi zao zinafanya kila linalowezekana kuimarisha uhusiano wao wa kibiashara na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, licha ya Marekani kuchukua hatua ya upande mmoja ya kujiondoa kwenye mapatano hayo ya kimataifa.
-
Kutangazwa msimamo wa Russia wakati wa kukaribia uzinduzi tarajiwa wa mpango wa "Muamala wa Karne"
May 20, 2019 03:34Utawala wa Kizayuni wa Israel kwa kuzingatia himaya na uungaji mkono wa pande zote wa Rais Donald Trump wa Marekani umekuwa ukitekeleza mashinikizo ambayo hayajawahi kushudiwa dhidi ya wananchi madhulumu wa Palestina na kufanya mambo kinyume kabisa na sheria za kimataifa.
-
Erdogan: Uturuki kuunda na Russia mifumo ya makombora ya S-500
May 19, 2019 08:19Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki amesema kuwa nchi yake na Russia kwa pamoja zitaunda mifumo ya makombora ya S-500 baada ya mpango wake wa awali wa kunununua mfumo wa makombora wa S-400 kutoka Moscow kuzusha mivutano.
-
Putin: Leo hii Iran ndiyo yenye miradi iliyo wazi zaidi ya nyuklia duniani
May 15, 2019 22:28Rais Vladimir Putin wa Russia amesema kuwa, tangu yalipofikiwa mapatano ya nyuklia ya JCPOA mwaka 2015 hadi hivi sasa, Iran imekuwa ndiyo nchi yenye miradi iliyo wazi zaidi ya nyuklia duniani.
-
China, Russia, Ufaransa na Ujerumani zatoa radiamali zao kufuatia tangazo la Iran
May 08, 2019 09:20Russia, China, Ufaransa na Ujerumani ambazo ni katika nchi tano zilizosalia katika mapatano ya nyuklia ya JCPOA zimetoa radimali kufuatia uamuzi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran wa kusimamisha kwa muda utekelezaji wa baadhi ya ahadi zake kuhusu mapatano hayo, ikiwa ni mwaka mmoja baada ya Marekani kujitoa kwa upande mmoja katika mapatano hayo muhimu ya kimataifa.
-
Jamhuri ya Kiislamu ya Iran yatoa mkono wa pole kwa serikali na raia wa Russia kutokana na ajali ya ndege
May 06, 2019 23:42Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Sayyid Abbas Mousavi amesema kuwa Iran inatoa mkono wa pole kwa serikali na raia wa Russia kufuatia ajali ya ndege ya abiria ya nchi hiyo.