Russia: Misimamo ya Moscow mkabala na Tehran haijabadilika
https://parstoday.ir/sw/news/world-i53699-russia_misimamo_ya_moscow_mkabala_na_tehran_haijabadilika
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia amesisitiza kuwa misimamo ya nchi hiyo mkabala na Iran haijabadilika baada ya Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Marekani kufanya ziara mjini Moscow.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 24, 2019 23:32 UTC
  • Russia: Misimamo ya Moscow mkabala na Tehran haijabadilika

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia amesisitiza kuwa misimamo ya nchi hiyo mkabala na Iran haijabadilika baada ya Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Marekani kufanya ziara mjini Moscow.

Maria Zakharova amesema kuwa misimamo ya nchi yake kuhusu Iran baada ya kufanyika mazungumzo kati ya Mike Pompeo Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Marekani na waziri mwenzake wa Russia Sergei Lavrov pamoja na Rais Vladimir Putin wa nchi hiyo haijabadilika. Maria Zakharova ameongeza kuwa uhusiano wa Russia na Iran haufungaman na mawasiliano yanayofanywa kati ya Moscow na nchi nyingine na kwamba ziara ya Pompeo mjini humo pia haijabadili misimamo ya Russia.  

Mike Pompeo (kushoto) akiwa na Sergei Lavrov mjini Moscow 
 

Kama alivyobainisha Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia Tehran ilitangaza nia yake ya kusimamisha utekelezaji wa sehemu ya makubaliano ya nyuklia ya JCPOA katika kujibu vikwazo vya Marekani. Amesema kwa mujibu wa sheria za kimataifa Iran ina haki ya kuchukua hatua kama hiyo kulingana na azimio nambari 2231 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ambalo mwaka 2015 liliidhinisha makubaliano hayo ya nyuklia. 

Mwaka mmoja uliopita serikali ya Marekani iliamua kujitoa katika makubaliano hayo ya kimataifa kufuatia agizo la Rais Donald Trump wa nchi hiyo; na kisha ikaanzisha tena vikwazo vyote vya nyuklia dhidi ya Iran katika awamu mbili yaani muda wa siku 90 na 180.