-
Iran, China na Russia zafanya luteka ya pamoja katika Bahari ya Oman
Mar 16, 2023 07:55Vikosi vya majini vya Iran, Russia na China vinaendelea na mazoezi ya pamoja ya kijeshi katika Bahari ya Oman, huo ukiwa ni muendelezo wa juhudi za nchi tatu hizo za kuimarisha ushirikiano wa majeshi yao ya baharini.
-
Russia yasema itajibu chokochoko zozote tarajiwa za Marekani
Mar 16, 2023 06:23Kufuatia makabiliano ya kijeshi kati ya Russia na Marekani katika anga ya Bahari Nyeusi Jumanne ya juzi, Wizara ya Ulinzi ya Russia imesisitiza kuwa, taifa hilo litatoa majibu muafaka kwa uchokozi wowote tarajiwa wa Marekani.
-
Makabiliano ya kijeshi yasiyo ya kawaida kati ya Russia na Marekani katika anga ya Bahari Nyeusi
Mar 16, 2023 00:45Kituo cha kamandi ya Marekani barani Ulaya kimetangaza kuwa Jumanne asubuhi, ndege ya kivita ya Russia aina ya Sukhoi Su-27 iligongana na ndege isiyo na rubani (droni) ya Marekani aina ya MQ-9 Reaper katika anga ya Bahari Nyeusi, na kupelekea droni hiyo kuanguka kwenye maji ya kimataifa.
-
Mazoezi ya pamoja ya kijeshi kati ya China, Iran na Russia yaanza katika Bahari ya Oman
Mar 15, 2023 04:28Wizara ya Ulinzi ya China imetangaza kuwa, mazoezi ya pamoja ya kijeshi ya majini yanayoishirikisha nchi hiyo, Iran na Russia yatafanyika katika Bahari ya Oman kuanzia leo Jumatano hadi Machi 19.
-
Droni ya US yaanguka ikidaiwa kugongana na ndege ya kivita ya Russia, Moscow yakanusha
Mar 15, 2023 03:53Jeshi la Marekani limedai kuwa ndege ya kivita ya Russia ilinasa propela ya ndege moja ya kijasusi isiyo na rubani ya nchi hiyo na kuifanya ianguke kwenye Bahari Nyeusi jana Jumanne katika makabiliano ya kwanza ya moja kwa moja kati ya madola hayo mawili tangu Russia ilipoanzisha operesheni za kijeshi nchini Ukraine mwaka mmoja uliopita.
-
Russia: Malengo yetu Ukraine yataweza kufikiwa kwa operesheni za kijeshi tu
Mar 15, 2023 00:35Msemaji wa ofisi ya rais wa Russia amesema malengo ya nchi hiyo nchini Ukraine yanaweza kufikiwa kupitia operesheni za kijeshi tu.
-
Watoto karibu 50 kutoka familia za magaidi wa Daesh kuhamishiwa Moscow
Mar 12, 2023 23:18Watoto karibu 50 wa familia za masalia ya magaidi wa kundi la kitakfiri la Daesh (ISIS) wamehamishwa katika mji mkuu wa Russia, Moscow.
-
Russia: Madai ya New York kuhusu milipuko ya Nord Stream ni upotoshaji
Mar 08, 2023 03:10Russia imetangaza kuwa madai yaliyotolewa na gazeti la New York Times kuhusu milipuko iliyotokea kwenye mabomba ya kusafirisha gesi ya Nord Stream ni ya kubuniwa na opotoshaji wa makusudi unaofanywa na wale wanaopinga uchunguzi wa kisheria kuhusu shambulio hilo.
-
Russia: Marekani ndiyo sababu kuu ya kurefuka vita nchini Ukraine
Mar 07, 2023 22:54Msemaji wa ofisi ya rais wa Russia amesema, Marekani ndiyo sababu kuu ya kurefuka vita vinavyoendelea nchini Ukraine.
-
Marais Raisi na Putin wazungumzia uhusiano wa kiuchumi wa Iran na Russia
Mar 06, 2023 23:29Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Ebrahim Raisi na mwenzake wa Russia, Vladimir Putin wamesisitizia umuhimu wa kuchukua hatua za kuimarisha zaidi uhusiano wa kiuchumi kati ya nchi mbili hizi.