Pars Today
Qatar imethibitisha kuwa kiongozi wa nchi hiyo Sheikh Tamim bin Hamad Al Thani atahudhuria mkutano wa 41 wa wakuu wa nchi wanachama wa Baraza la Ushirikiano la Ghuba ya Uajemi (GCC) unaofanyika leo katika mji wa Al-Ula nchini Saudi Arabia.
Mamluki wanaoungwa mkono na Saudi Arabia wamevamia sherehe ya harusi katika mji wa bandarini wa Al Hudaydah nchini Yemen na kuua watu wasiopungua watano na kuwajeruhi wengine kadhaa wakiwemo wanawake saba.
Katika mwendelezo wa siasa za White House zinazolenga kuuza silaha zaidi; Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Marekani imetangaza kuwa imeafiki kutekelezwa mikataba ya kuziuzia silaha Misri, Kuwait na Saudi Arabia.
Gazeti la Washington Post limeripoti kuwa Saudi Arabia na Misri zimo kwenye orodha ya nchi hatari sana kwa waandishi habari katika mwaka huu wa 2020.
Serikali ya Marekani imeamua kutoa kibali cha kuruhusu kuiuzia Saudia mabomu; hatua ambayo imepingwa vikali na wabunge wa chama cha Democrat.
Wanazuoni zaidi ya 12 wa Kiislamu wa madhehebu ya Shia wanashikiliwa bila kufunguliwa mashtaka nchini Saudi Arabia huku ufalme huo ukishadidisha ukandamizaji wa jamii za waliowachache nchini humo.
Duru za habari zimearifu kuwa, Saudi Arabia imebadilisha vitabu vya masomo ya wanafunzi wa shule nchini humo kulingana na matakwa ya utawala haramu wa Kizayuni.
Baadhi ya duru za kuaminika zimeripoti kuwa mrithi wa ufalme wa Saudi Arabia na mwenzake wa Imarati (UAE) wamefanya kikao cha faragha cha kuzungumzia kadhia ya Qatar.
Mwanaharakati mwanamke mtetezi wa haki za binadamu nchini Saudi Arabia ambaye amefungwa jela kwa kupigania kuondolewa marufuku ya wanawake kuendesha gari sasa anakabiliwa na mashtaka ya kufanya ujasusi kwa manufaa ya baadhi ya nchi za Ulaya.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema, makundi yote ya kigaidi katika eneo la Asia Magharibi yamepewa mafunzo ya elimu katika madrasa zinazofadhiliwa kifedha na Saudi Arabia.