Saudia yabadilisha vitabu vya masomo ili kuuridhisha utawala wa Kizayuni
(last modified Mon, 21 Dec 2020 02:59:07 GMT )
Dec 21, 2020 02:59 UTC
  •  Saudia yabadilisha vitabu vya masomo ili kuuridhisha utawala wa Kizayuni

Duru za habari zimearifu kuwa, Saudi Arabia imebadilisha vitabu vya masomo ya wanafunzi wa shule nchini humo kulingana na matakwa ya utawala haramu wa Kizayuni.

Televisheni ya al Alam imelinukuu shirika la habari la Times News na kuripoti kuwa, masuala yanayohusiana na chuki dhidi ya Uyahudi na Uzayuni yatapunguzwa sana katika vitabu vya masomo katika shule nchini Saudi Arabia mwaka ujao wa masomo. 

Ripoti ya televisheni ya al Alam imeongeza kuwa,  Saudia imeanza kuchukua hatua za kuandaa mazingira ya kutangaza uhusiano wa kawaida kati yake na utawala wa Kizayuni wa Israel kwa mujibu wa sera kuu zilizoanishwa na Marekani. Hii ni katika hali ambayo kitambo nyuma baadhi ya duru zilitoa taarifa ya kuweko uwezekano wa Saudi Arabia kuanzisha uhusiano wa kawaida na Israel na kuitaja hatua hiyo kuwa ni sehemu nyingine ya matukio ya kieneo kufuatia hatua ya nchi za Imarati, Bahrain, Sudan na Morocco ya kuanzisha uhusiano wa kawaida na Israel.  

Magaidi wa mtandao wa al Qaida ulioasisiwa na Saudi Arabia 

Itakumbukuwa kuwa, wakati Umoja wa Kisovieti ulipoivamia Afghanistan, Saudi Arabia pia iliongeza nadharia za Kiwahabi katika vitabu vyake vya masomo ambazo zilikuwa zikichochea vita na Urusi ya zamani chini ya usimamizi wa Marekani. Matokeo ya fatwa na nadharia hizo za Saudia ilikuwa ni kuasisiwa magenge ya kigaidi kama vile al Qaida, Daesh (ISIS) na Jabhatul Nusra. 

Tags